Mbunge wa kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Ester Bulaya na Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob na wanachama wengine 25 wa Chadema wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa tuhuma za kufanya vurugu katika gereza la Segerea.
Baada ya kupandishwa Kizimbani Mahakamani hapo wamesomewa mashtaka 7 yakiwemo ya kuharibu geti kuu la mlango wa kuingilia gereza la Segerea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na CHADEMA, katika ukurasa wake wa Twitter, watuhumiwa hao walitakiwa kuripoti Polisi leo, lakini wamepelekwa Mahakamani.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment