Breaking

Thursday, April 2, 2020

Aliyeshushiwa kichapo na Ebitoke afunguka mapya..Full Vituko


Mrembo Precious maarufu kama Beyonce, ambaye alipigana na Ebitoke kisa kugombania penzi la  Yusuph Mlela, amefunguka kuwa wanaume wengi wamekuwa wakimjaribu kwa milioni tano ili kumuona kama ni mdangaji.


Akipiga stori na eNewz ya East Africa TV, Beyonce amesema huwa anasumbuliwa na wanaume kupitia Instagram na kumtaka adange kwa milioni tano ila huwa anawakatalia.

"Sijawahi na siwezi kudanga, napata ujumbe mwingi sana wa Instagram "DM" kutoka kwa wanaume, maana wameona nimeacha kutrend wanadhani mimi ni walewale, kiwango cha juu wanachonitajiaga ili kunitaka kimapenzi ni milioni 3 hadi 5, mimi umri wangu bado mdogo sana, naweza kufanya kazi na nikaishi maisha mazuri ila sio kudanga" ameeleza Beyonce.

Tazama mahojiano hayo zaidi kupitia video hii hapa chini.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment