Breaking

Friday, April 3, 2020

Amber Lulu Alia Kuwa na Nyota ya Mchepuko


Msanii Amber Lulu amefunguka na kueleza kuwa, huwa anatamani angekuwa anamiliki mume wake mwenyewe ili hata siku akimpost katika mitandao ya kijamii aweze kumuita mke.Amber Lulu ameweka wazi hilo kufuatia post ya picha na maelezo aliyoyaweka katika mtandao wa Instagram ambapo ameandika.

"Mimi natamani kuwa na mume wangu mwenyewe, ambaye hata nikimpost kama Queen Darleen ili na mimi aniite mke wangu, ila sisi wengine tuna nyota ya kuwa "sidechick" michepuko" ameandika Amber Lulu.

Katika maisha yake ya mahusiano ya kimapenzi msanii huyo tayari alishakuwa na Young Dee pamoja na Prezzo kutoka nchini Kenya.

Siku za hivi karibuni kulikuwa na tetesi za Amber Lulu kuwa kwenye mahusiano na msanii  Otike kutokea nchini Nigeria, baada ya ukaribu wao kuwa mkubwa  na kumpost katika mtandao wa Instagram.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment