Bibi huyo ambaye amejulikana kwa jina la Olive Veronesi, kutokea Mji wa Pittsburgh, Pennsylvania iliyopo Marekani, amefanikiwa kupata anachokitaka baada ya kuchangiwa makopo 150 ya bia.
Kwa mujibu wa CBS Pittsburgh, Bibi huyo Olive Veronesi amesema anapenda sana bia kwa sababu ina virutubisho na lazima anywe kila ifikapo usiku.
"Nilikuwa nimebakiwa na makopo 12 ya bia, lazima niwe na bia kila ifikapo usiku, halafu unajua bia ina vitamini na ni nzuri kwako kama hautazidisha" amesema Bibi huyo.
Chanzo CNN.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment