Mmiliki wake anasema aliposogelea mahali alipokuwa ndipo alipoona mguu wa mtoto mchanga ukitokezea juu ya ardhi.
Wanakijiji walimkimbiza mtoto hospitalini ambako madaktari walimuogesha na kutangaza kuwa alikuwa mzima wa afya.
Mmiliki wa mbwa Ping Pong , Usa Nisaikha, anasema mguu wa mbwa hake hauna nguvu baada ya kugongwa na gari.
Aliliambia gazeti la Khaosod : ” Ninamtunza kwasababu ni mwaminifu sanana kila mara huwa ananisaidia ninapokwenda shambani kuwahudumia mifugo wangu. Anapendwa sana na kijiji kizima.
Inashangaza.”
Mbwa Ping Pong amekuwa mlemavu wa mguu tangu alipogongwa na gari
Mama yake mtoto huyo mchanga amekwishashtakiwa kwa kumtelekeza na kujaribu kumuua.
Panuwat Puttakam, afisa lkatika kituo cha Chum Phuang, alililiambia gazeti la the Bangkok Post kuwa sasa mama huyo anahudumiwa na wazazi wake pamoja na mtaalamu wa kisaikolojia.
Alisema anajutia matendo yake.Wazazi wa msichana wameamua kumlea mjukuu wao.
By Ally Juma.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment