Breaking

Thursday, April 9, 2020

Huyu Hapa Ndio Mtoto wa Hadija Koppa Aliyekula Shavu WCB Wasafi....

Huyu Hapa Ndio Mtoto wa Hadija Koppa Aliyekula Shavu WCB Wasafi....
Lebo kubwa ya muziki hapa Bongo inayomilikiwa na mkali wa bongo fleva Diamond Platinumz Wasafi Classic Baby (WCB) leo imemtambulisha msanii mpya ambapo amekaribishwa na samba mwenywe amemkaribisha.

Msanii aliyesajiliwa ni Zuchu ambaye ni mtoto wa Hadija Koppa ambaye ni sehemu ya wasanii walioimba nyimbo ya Super Woman.

Katika ukurasa wa Istagramu wa Kampuni hiyo walimkaribisha wakisema Ni mtoto wa Malkia Mwenye Sauti ya Kasuku “Amepikwa akapikika Sasa Ni Muda wa Dunia Kufurahia kipaji Hiki Kipya kutoka Tanzania”.

“Tafadhali kwa Heshima na Taazima Tunawaomba Watanzania Mumpokee na Kusheherekea Kipaji chake”.

Msanii Diamond aliposti Zuchu na kumkaribisha kundini huku akiwatka wapenzi wa muziki nchini kumfuatilia msanii huyo katika mitandao yake ya kijamii.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment