Breaking

Thursday, April 9, 2020

Khadija Khopa atoa ya moyoni baada ya mwanaye kutambulishwa WCB


Malkia wa Mipasho nchini, Bi Khadija Omar Kopa  ameeleza kwa hisia kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwa haamini kilichotokea kwa binti yake baada ya kutamburishwa kwenye lebo ya WCB.

Khadija Kopa aitaja 'Subra' kuwa ni moja ya siri ya mafanikio ya binti yake @officialzuchu kufikia hatua ya kuingia mkataba wa kibiashara na lebo ya WCB ya msanii Diamond Platnumz.

Kupitia instagramu yake ameandika;

"Yani sijalala kwa amani kwa furaha mana kama siamini,tumemfuta sana machozi mpaka leo kafikia hapa Basi Ashukuriwe M/mungu kwa neema hii".

Zuchu ametambulishwa jana Jumatano Aprili 8, 2020 na Diamond ambaye ni mkurugenzi wa lebo hiyo na kufanya idadi ya wasanii wa WCB kufikia sita. Unaweza kusema Zuchu ametambulishwa rasmi kwa kuwa alikuwa katika lebo hiyo tangu mwaka 2018.

Itakumbukwa, Zuchu amewahi kushiriki shindano ya kusaka vipaji vya muziki barani Afrika mwaka 2016 liitwalo Tecno Own The Stage ambalo pia msanii Faustina Charles maarufu Nandy naye alishiriki na kupata Sh36 milioni baada ya kuwa mshindi wa pili.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment