Breaking

Monday, April 6, 2020

Mbaroni kwa Kusambaza Taarifa za Uongo Kuhusu #Coronavirus


MTU mmoja aliyetambulika kwa majina ya African John Mlay (58) Mkazi wa Kiboroloni, Moshi anashikiliwa na  polisi mkoa wa Kilimanjaro kwa tuhuma za kuchapisha na kusambaza mtandaoni taarifa za uongo kuhusu ugonjwa wa #Covid19.

 

Kaimu Kamanda wa Polisi, James Manyama, amesema mtuhumiwa huyo alichapisha taarifa yenye takwimu za wagonjwa tofauti na zile za Wizara ya Afya katika mitandao ya Twitter, Instagram na WhatsApp.

 

Taarifa hiyo iliyochapishwa Aprili 4 ilisema, “Ni kwa nini Serikali ya Tanzania inaficha sana takwimu za ugonjwa wa corona? Kumekuwa na usiri mkubwa mno wa ugonjwa huu wa corona…ukweli uliopo mpaka sasa Tanzania kuna wagonjwa 200+ wa corona na mpaka sasa waliokufa na corona ni wagonjwa wanne na hii yote imefanywa siri ya Serikali na idara zake za takwimu.”

 

Kamanda Manyama amesema taarifa hizo ni upotoshaji na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani hivi karibuni.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment