Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Bunge, Freeman Mbowe, amesema kuwa suala la Corona halijapewa uzito unaostahili huku akishauri kuundwa kwa kikosi kazi cha Taifa kwa ajili ya kuangalia athari za uchumi za ugonjwa huo.
Amebainisha kuwa sekta ya utalii imeanguka kwa asilimia 99 na kwamba kuna makampuni yamefungwa huku mapato ya nchi yatapungua kwa asilimia 40 kwa miezi sita ijayo.
“Kumekuwa na kauli tofauti,mikusanyiko ambayo haifai na kwamba kuna mikusanyiko ambao wakuu wa mikoa ndio wamekuwa wakiifanyaWanakusanya watu, wanahutubia watu kwamba ugonjwa uko mbali hii ni hatari,”amesema.
Ameongeza “Ningetamani tumesikilize Rais, Waziri Mkuu na Waziri wa Afya kama
nchi ikienda kwa kila kiongozi kutoa taarifa ugonjwa huu utawafikisha mahali pabaya.”
Amesema jambo hilo linahitaji kikosi cha Taifa kwa ajili ya kuangalia athari za uchumi na kijamii na pia kuangalia vipaumbe vya Taifa hivi sasa ni vipi.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment