Breaking

Thursday, April 2, 2020

Mgonjwa wa Corona Agoma Kuwekewa Mashine ya Kupumulia Afariki, Aacha Ujumbe MzitoSuzanne Hoylaerts mwenye umri wa miaka 90 ambaye alikuwa na ugonjwa wa virusi vya Corona nchini Ubelgiji amefariki baada ya kukataa kuwekewa mashine.

Mgonjwa huyo alikuwa anawekewa mashine kwa ajili ya kumsaidia kupumua.

Suzanne aligoma kuwekewa mashine hiyo huku akitaka mashine hiyo ikawasaidie wagonjwa wingine.

Kabla ya kukutwa na umauti alidai kuwa ameishi maisha mazuri tayari wapatiwe wengine hiyo mashine.

“Nimeshaishi maisha mazuri tayari, ihifadhi kwa ajili ya wengine wenye umri mdogo kuliko mimi,” alisema awali kabla ya kufa.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE 

No comments:

Post a Comment