Breaking

Thursday, April 9, 2020

Niliamua Kutembea Kimapenzi na Mama Yangu wa Kambo Kulipiza Kisasi

Iwapo ulifikiri umeyaona na kuyasikia basi mengi yapo ambayo utayafahamu kwa mara ya kwanza papa hapa .

Wakati mwingi inakuwa vigumu kwa watoto kukubali kwamba baba yao ameoa mke wa pili kando na mama yao .Wengine hukubali hali ilivyo na kuendelea na maisha lakini hasira za Edward Ekuwom hazikumwezesha kusalia kimya wakati babake mzazi alipoamua kuoa mke wa pili na kutengana na mama yao . Kilichowahamakisha yeye na dada zake wawili ni kwamba mzee wao aliamua kuoa msichana ambaye alikuwa na umri sawa na wao.

‘ Yule msichana alikuwa rika langu na tungekutana club ,ningemkatia’ anasema Edward.

Wakati baba yao alipooa msichana huyo alihama kutoka nyumbani kwao Lodwar na kwenda Kitale ambako alimfungulia mke wake huyo wa pili biashara . Edward na dada zake waliendelea kushangaa mbona baba yao kaamua kumwoa mwanamke mwingine ilhali mama yao hakuwa amemkosea lolote na ktika macho yao ,mama yao hakuwa na kasoro yoyote na hivyo basi baba yao hakustahili kumuacha . Huku dada zake wakubwa ambao tayari walikuwa wameolewa wakikubali jinsi mambo yalivyokuwa ,Edward katika moyo wake alikuwa na makovu na akakula njama mmwenyewe ya kulipisha kisasi ili kumpa somo baba yake .

‘Sikutaka kuendelea kumuona mamangu kama victim,I decided my da had to pay.Kila siku ilikuwa nafikiria kuhusu kumfanyia kitu ambacho kitamfanya asikie uchungu pia’ anasema Edward .

Aliporudi Nairobi kwa masomo kwa sababu alikuwa mwanafunzi wa chuo kimoja kikuu Edward alikuwa akizungumza na babake lakini kisiri alikuwa ameficha machungu . Aliamua kwamba njia ya kumuadhibu babake itakuwa kumtongoza yule mamake wa kambo ambaye alikuwa msichana wa rika lake . Edward alianza kujifanya mzuri na hata akawatembelea babake na mke wake mdogo huko Kitale wakati wa likizo . Hakuonyesha kwamba alikuwa na hila na alianza kujenga uhusiano wa karibu na mamake wa kambo .muda sio mfupi walibadilishana nambari za simu na kuanza kuwasiliana mara kwa mara ,hasa kupitia whatsapp.

‘Babangu hakujua atapigwa na radi kutoka wapi,nilikuwa nimempangia na plan yangu ilianza kunoga’ anasema Edward

Kama mchezo , Edward alianza kumtongoza mamake wa kambo . bila kujua njama ya Edward ,mama kambo alijipata kaanza kumuambia Edward mambo ya kumpenda na kumtaka .Ikawa sasa safari imeiva kasi kweli .Kilichobaki ni kupanga muda na eneo la mchezo kusakatwa! Mama kambo hata ndiye aliyeanza kupendekeza uwezekano wake kusafiri kuja Nairobi kumuona Edward ndiposa wapate fursa ya kuwa wao wawili pekee yao.

Siku ilipangwa , mama mtu akaja Nairobi kumuona Edward na hayawi hyawi ..huwa! kwa sababu Edward alikuwa akiishi katika hostel ya wanafunzi ,mtaani south C,mamake kambo alikodi danguro walikolala usiku huo mtaani Ngara . Edward alishiriki mapenzi na mamake wa kambo ,mke mdogo wa babake na hadi leo hana majuto kwa sababu lengo lake lilikuwa kumkwaza babake . Maskini mamake wa kambo hakujua anatumiwa tu kama karata katika mchezo mrefu wa makovu ya familia ya Ekuwom . Kampenda Edward na hata alikuwa ameanza kumueleza kuhusu njama ya kumtoroka babake ili waanze maisha pamoja sehemu ya mbali !

Alijipata katika njia panda kwa sababu kwa upande mmoja alikuwa anataka kumpa babake funzo na kwa upande wa pili alikuwa ameanza kumhurumia mamake wa kambo . alishindwa atafanyaje ili isigunduliwe na yule mamake wa kambo kwamba uhusiano wao muda wote huo ulikuwa feki na msingi wake ulikuwa kulipiza kisasi . Edward alichukua picha za jumbe walizokuwa wakibadilishana na mamake wa kambo na kumpa rafiki yake ,aliyezituma kwa simu ya babake .

Hapo ndipo moyo wake ulipotulia kwa sababu mzee watu alifoka na kutokwa ukemi wote ulioweza kumtoka siku ile -Kahawadaiwa kimapenzi na msichana ambaye alikuwa na uhusiano wa pembeni! Mzee wa watu alijaribu kurejea kwa mamake Edward lakini mama ya watu alikuwa ashaamua kusalia na amani yake alivyokuwa .hakutaka tena kuishi na ‘msaliti’ kama mzee wa watu alivyoitwa sasa . Babake Edward hakujua kwamba mke wake wa pili alikuwa na uhusiano na mwanawe. Wakati mwingine siri isalie siri ili pawepo amani ila kwa machungu aliopitia mamake Edward ,hangeweza kujisamehe iwapo hangechukua hatua . Mambo hayo!

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment