Breaking

Saturday, April 4, 2020

Roma Avunja Ukimya wa Miaka Miwili INSTAGRAM..."Nimemkamata Aliyekuwa Anatumia JINA Langu Instagram"Msanii wa HipHop Roma Mkatoliki ameeleza kuwa hakuwepo katika mtandao wa Instagram kwa muda wa miaka miwili baada ya kudukuliwa "Hacked" na wadukuzi ambapo hakuweza kuipata tena.

Roma amesema kipindi chote  ambacho hakuwa katika mtandao huo kuna mtu alikuwa anatumia jina lake ambaye hamjui kwa kujitambulisha kwa watu kwamba yeye ndiyo Roma, ila aliwahi kumshataki kwenye vyombo vya usalama.

Kwa bahati nzuri amefanikiwa kuipata akaunti yake ya mtandao huo ambapo ameeleza,

"Kwa takribani kipindi cha miaka 2 (2018 - 2020) sikuwepo na akaunti ya Instagram, akaunti yangu ilikuwa "hacked" na sikuweza kufanikiwa kuipata mpaka leo hii, kipindi hicho cha mwaka 2018 alitokea mtu nisiyemfahamu akafungua akaunti  na kuendelea kuitumia na akiaminisha watu na kuwarubuni kuwa ni mimi" 


"Baada ya kuhangaika kwa muda mrefu, mimi na timu yangu tukishirikiana na Vyombo vya usalama tumefanikiwa kumpata mtu huyo na kuichukua rasmi akaunti hii, na mtuhumiwa yuko chini ya ulinzi wa vyombo vya usalama" ameongeza 

Mengine zaidi aliyoyaeleza tazama kwenye post hapam chini.
View this post on InstagramKwa Takribani Kipindi Cha Miaka 2 (2018 - 2020) Mimi Sikuwepo Na Sipo Na Account Ya "INSTAGRAM" Account Yangu Ilikuwa HACKED Na Sikuweza Kufanikiwa Kuipata Mpaka Leo Hii, ingawa Mpaka Sasa Account Hiyo Wameibadilisha Jina Na Kwa Sasa Inajulikana Kama @ireneuwwoya8 Lakini Sijafanikiwa Kuipata Na Simjui Anayeitumia Ni Nani!! Kipindi Hicho Hicho Cha Mwaka 2018 (Kipindi Ambacho Account Yangu Hiyo Iko Hacked) Alitokea Mtu Nisiemfahamu Akafungua Account Na Kujiita @roma_zimbabwe Na Baadaye Account Hiyo Ikawa Verified ( Alifoji Vitambulisho Vyangu Kwa Maelezo Yake) Na Akaendelea Kuitumia Akiaminisha Watu Na Kuwarubuni Kuwa Ni Mimi!! Nimekuwa Nikilisema Mara Kwa Mara Hili Kwenye Interviews Zangu MbaliMbali Kwa @millardayo @lilommy @Cloudsfmtz #EastAfricaTvandRadio @efmtanzania @wasafitv Na Media Nyingine nyingi Kuwa Mimi Sipo INSTAGRAM Na Huyo Mtu @roma_zimbabwe Siyo Mimi na Wala Simfahamu. Kwa Bahati Nzuri Niliwahi KumReport Mapema Kabisa Kwenye Vyombo Husika Vya Usalama. Baada Ya Kuhangaika Kwa Muda Mrefu, Mimi Na Team Yangu Tukishirikiana Na Vyombo Hivyo, Hatimaye Tumefanikiwa Kumpata Mtu Huyo Na Kuichukua Rasmi Account Hii!! Na Mtuhumiwa Yuko Chini Ya Ulinzi Wa Vyombo Vya Usalama. Nichukue Nafasi Hii Kuwaomba Radhi Mashabiki Zangu Na Watu Wote, (Followers) Kuwa Vyote Vilivyopostiwa Kipindi Hiko Chote, Sikuwa Mimi!! Najua Wengi Walirubuniwa Kwa Namna Moja Ama Nyingine, Kwenye DM/Comments na Kwingineko Wakidhani Na Kuamini Ni Mimi Lakini Narudia Tena SIKUWA MIMI!! Najua Wengi Walikwazika Na Baadhi Ya Post na Taarifa Alizokuwa Anapost (Matangazo Ya Waganga Wa Kienyeji Na Nguvu Za Dawa Za Kiume N.K ) Wakidhani Ni Mimi. SIKUWA MIMI!! Mtu Huyu Taarifa Na Habari Zangu Nyingi Alikuwa Akizitoa Twitter Ambako Ndio Mtandao Hasa Ninaotumia @Roma_mkatoliki Pia Alikuwa Akizipata Kwenye Media (Radio/Tv/Onlines) Na Vyanzo Mbali Mbali Na Kuzileta INSTAGRAM. Nimalize Kwa Kusema Kuwa, Kwa Sasa Account Hii @roma_zimbabwe Nimeichukua Mimi Rasmi Baada Ya Kufuta Kila Kitu (Naanza Upya) Na Nitakuwa Naitumia Kuanzia Leo Katika Kazi Zangu za Sanaa Na Mambo Yangu Binafsi Kama Official Account Ya #ROMAmkatoliki.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment