Hata hivyo, alisema kuwa Bunge liliahirisha kikao kimoja kwa ajili ya kuomboleza kifo cha mbunge huyo.
“Mazingira ya sasa hayaruhusu kufanya zoezi hilo. Kwahiyo, hatutaweza kumleta mwenzetu hapa kwa sababu ya hali halisi tuliyonayo,” amesema Spika Ndugai.
“Maelezo mengine tutayapata kesho baada ya kuwa tumemaliza mazungumzo kati ya ofisi ya Bunge na familia ya marehemu wakati Serikali nayo ikijiandaa kusaidia pale ambapo tunaweza kuomba msaada wowote ambao utahitajika,” aliongeza.
Katika hatua nyingine, Spika aliwasihi wabunge kuhakikisha kuwa wanapojisikia hali isiyo ya kawaida kiafya wasijilazimishe kufika bungeni kwa hofu ya kutokiuka utaratibu, kwani mazingira ya sasa yanafahamika.
Dkt. Rwakatare ambaye alikuwa Askofu Kiongozi wa Kanisa la Mlima wa Moto alifariki alfajiri, Aprili 20, 2020 akiwa na umri wa miaka 70. Mwanaye alieleza kuwa alifariki kutokana na tatizo la moyo.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment