Breaking

Sunday, April 5, 2020

Ugonjwa wa Corona Wamtia Simanzi Mbwana Samatta

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars anayecheza soka la kulipwa katika club ya Aston Villa ya England Mbwana Samatta ameonekana kuwa miongoni mwa watu wanaopata mawazo sana wakati huu wa virusi vya corona.

“Haya maisha ya kuwa tu ndani yamenifanya niwafikirie zaidi wenzetu waliopo magerezani… nina uhuru wa kwenda supermarket na wa kula chakula ninachokitaka achana na tv, simu, kitanda chenye joto😁(if you know what I mean) wenzetu hawana hivi vitu..tuwaombee sana wanayopitia ni magumu”>>> Samatta

Samatta amejiunga na Aston Villa Janury 2020 akisaini mkataba wa miaka minne na nusu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji hadi sasa amecheza game 6 na kufunga magoli 2 kabla ya Ligi kusimama.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment