Breaking

Wednesday, April 8, 2020

Usikubali Kuogopa Kumuonyesha Mke au Girlfriend Wako Unampenda Kisa Unaogopa Washkaji Watakuona Bwege


Usikubali kuogopa kumuonyesha mke wako au girlfriend wako unampenda kisa unaogopa washkaji au ndugu watakusema umekaliwa naye. Ni tabia mbaya sana unakuta mtu mzima eti anajitamba mbele za wanaume eti "mimi bwana mwanamke hawezi niuliza niko wapi" sasa ndugu yangu wewe ndio ulimtongoza mwenyewe tena ulimsumbua hasa msichana wa watu leo hii anakupigia simu anakuuliza uko wapi unaanza kupanic. Tusifanye vitu ili kuwaridhisha washkaji huko viringeni...tufanye vitu kuwaridhisha wake zetu....

Imefikia wakati mwanaume usipokaa bar mpaka saa nane au saa saba usiku unaonekana bwege na ukiangalia ligi ya ulaya sebleni kwako na mke wako unaonekana bwege pia...au usipokua na demu wa nje eti wewe sio mjanja. huu ni upuuzu tubadilikeni jamani. ndio sikatai usikae na washkaji lakini usipitilize sasa.

Naona huruma sana unakuta mtu kavaa lipete likuuubwa la ndoa amekaa bar kwenye kiti anasinzia..jamani ?


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment