Nahodha na mabaharia sita wa Kichina wamekutwa na hatia ya kujaribu kuwaua Watanzania wawili kwa kuwatupa baharini karibu na mwambao wa KwaZulu Natal, mwezi uliopita kwa hofu ya kuambukizwa #CoronaVirus
Amiri Salamu(20) na Hassani Rajabu(30) walitoswa baharini wakiwa wamepewa ‘life jackets’ na chupa za maji wakaamriwa kuogelea. Siku tatu baadae waliokotwa katika Fukwe ya ZinkwaziCui Rongli amekutwa na hatia ya kutowaliporipoti wazamiaji hao, na kuwatendea tukio ambalo lingeweza kuwasababishia kifo. Amelipishwa faini ya $5,000 sawa na Tsh. Milioni 11.5 na wenzake wamelipishwa Tsh. Milioni 5.7Meli hiyo ilikuwa inatoka Durban, Afrika Kusini kuelekea Singapore
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment