Breaking

Tuesday, April 7, 2020

Zari: “Natoka Mara Mojamoja Sana, Nimejifungia”

Zari ambae ni miongoni mwa waliojifungia majumbani nchini South Africa ili kujikinga na corona amepaza sauti kuhamasisha Watu watulie majumbani kama hawana mizunguko inayowalazimu kutoka, hii yote ni kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona.

Kwenye live na followers wake Instagram Zari amesema anaamini kutulia na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima kutasaidia, anasema amekua akitoka mara chache kufata chakula na vitu vingine kwenye super market na kila anaporudi nyumbani hulazimika kupuliza dawa vya kutosha ili kujikinga.

Mpaka sasa Nchi ya South Africa ina Wagonjwa wa corona 1655 huku vifo vikiwa 11 ambapo Taifa hilo bado linapambana ili waweze kuwa na uwezo wa kupima Watu 30000 kwa siku.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment