Mtoto wa Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo ( Chadema), Dudley Mbowe, ametangaza kupona rasmi virusi vya Corona ikiwa ni baada ya kupatiwa matibabu kwa takribani siku 57.
“Baada ya siku 57 hatimaye nimekutwa sina maambukizi..Shukrani na heshima kubwa madaktari na wauguzi wa hospitali ya Temeke hawa ni nyota wa mchezo ” ameandika
Ikumbukwe kuwa Dudley alikuwa mmoja kati ya watu wa mwanzoni kabisa kukutwa na virusi vya corona nchini.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment