*Mwonekano, Asikwambie mtu mwonekano hasa body unasaidia sana kuigusa hadhira.
*Kujithaminisha, jifanye ghali sio wa rahisirahisi.
*Dance/Cheza, Hili hadhira inafurahishwa nalo sana!
*Life style ya kisanii.
*Mbinu kali katika kutafuta na kuyaona masoko ya muziki/bidhaa yako.
Jamaa ni msanii aliyekamilika kwa ninavyomtazama, anajua sana kizazi hiki kinataka nini kutoka kwa msanii/mburudishaji na anatupatia kwa kweli.
Hili limefanya karibu Media zote hasa hizi Online kujikuta zinahitaji mno habari za Diamond ili kujitengenezea wafuatiliaji wa media zao.
Yaani kwa sasa media isiyoandika au kuzungumzia Diamond na WCB kwa ujumla inajichelewesha yenyewe!!
Tukubali au tukatae lakini Diamond anabaki kuwa ndie alama au dira kwa upande wa burudani hasa ya kizazi kipya hapa Tanzania. Ni vile tu Sisi weusi tumeumbwa kuchukia wanaofanikiwa kuliko kujifunza kupitia kwao!
Big up Platnumz.
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment