Hivi karibuni Mwanamama zari the boss lady ametoa povu kubwa kwa baadhi ya watanzania wanaomfuatilia Sana maisha yake ingawa Zari ana mapungufu yake binafsi lakini kwa Hili povu aliyotoa nimemuunga mkono kwa asilimia 100 Na hii imekuja baada ya tetesi ya yeye kurudiana na diamond lakini pia kwa kuzungumziwa vibaya mwanaye Tiffah nimnukuu baadhi ya maneno aliyoongea
Akaongeza pia sijawahi kuona mtu mwenye Mafanikio anamchukia mtu mwingine mwenye Mafanikio Mara nyingi watu wenye wivu ambao Ni masikini ndio wanachukiwa watu matajiri Leo hii siwezi Mimi zari kutoka Africa eti nimchukie Oprah wa Marekani hata nikimchukia ninapata faida gani? Kwani itamzuia yeye asipate Mafanikio? Aliyepewa kapewa tu watanzania wanatakiwa wawe inspired badala ya kuwa na chuki.
NB: Hili suala la wivu alilolizungumzia Zari ndio tabia halisi walionalo Watanzania Jana wakati nimepanda daladala naenda sehemu fulani mbele ya daladala niliyopanda kulikuwa na mark x dereva wa hiyo gari alikuwa anaendesha taratibu dereva wa daladala niliyopanda akasema Hawa wakishapata vigari vyao vya mkopo wanatusumbua Sana barabarani imagine unakuta huyo dereva hata tu baskeli Hana alafu anaongea kauli Kama hizo sijui watanzania tuna shida gani? sometimes ndo maana watu hawapati Mafanikio kutokana na hizi tabia
HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE
No comments:
Post a Comment