Breaking

Wednesday, November 14, 2018

KUMBUKUMBU | INSANE COINCIDENCE TITAN:TITANIC | SEHEMU 2

                                           .com/proxy/

UTANGULIZI
Duniani kuna mambo ya ajabu sana,pengine huwezi hata kufikirikama yanaweza kutokea lakini yapo.Kwa wale ambao hawajui au hawaelewi wanaweza kukataa na kubisha sana lakini hiyo haiondoi ukweli wenyewe.Sote tunafahamu kwamba kuna matukio hujirudia na hii hiutwa sadfa,hii ikimaanisha kwamba tukio moja linaweza kufanana na tukio lingine kwa bahati tu [coincedence].Lakini kuna mfanano ambao kamwe hauwezi kuwa ni kujirudia kwa matukio [sadfa] au tukio kufanana kwa bahati [coincedence]....

Moja kati ya matukio ambayo yamewahi kulela maswali mengi sana katika vichwa vya watu ni tukio la kuzama kwa meli iliyoitwa TITANIC.Je ni kwanini tukio hili liliacha maswali sana vichwani mwa watu? Usipoteze muda,twende pamoja katika makala hii ambapo utaweza kusoma kwa makini matukio mawili kisha nawe utaamua kama ni sadfa,bahati au ni tukio ambalo lilipangwa....

Nitaanza kuelezea tukio la ajali ya Titanic hatua kwa hatua hadi ajali kisha nitaendelea na kile kinachoitwa hadithi ya Futillity...


INAHUSIANA: KUMBUKUMBU | INSANE COINCIDENCE TITAN:TITANIC | SEHEMU 1  

ENDELEA HAPA: MIAKA 14 KABLA YA AJALI KUTOKEA 
Miaka 14 kabla ya ajali hii kuliwahi kutokea mtunzi mmoja mahiri kabisa aliyewahi kutunga hadithi iliyoleta maswali mengi sana vichwani mwa watu kuhusiana na ajali hiyo niliyoielezea hapo juu,mtunzi huyu aliitwa Morgan Andrew Robertson..

Morgan Andrew Robertson ni mwandishi wa zamani wa vitabu ambaye alikuja kuwa maarufu sana baada ya ajali ya meli ya kifahari kabisa kwa wakati wake,Titanic kupata ajali mbaya iliyoondoka na roho za watu zaidi ya 1400.Ni kwanini mtu huyu alipata umaarufu huu na mtu huyu ni nani?

Morgan Andrew Robertson ni kijana aliyezaliwa September 30,1861 kutoka kwa watu wawili wanaliojulikana kama Andrew na Amelia Robertson.Baba yake Robert alikuwa ni kiongozi wa meli na alikuwa akimchukua mwanaye kila mara anapofunga shule na kusafiri naye kwenye safari zake za majini na ndipo hapo Robert alipoanza kupenda na kupata uzoefu wa vurugu za kwenye maji....

Alipofikisha miaka 16 alikuwa anapenda sana safari za majini pamoja na hadithi za kwenye safari za kwenye maji.Aliendelea hivyo na alipomaliza shule alifanya kazi mbali mbali kabla hajaanza kuandika hadithi mbali mbali na nyingi zikiwa ni za habari za kwenye safari za baharini akihusisha meli....

Miongoni mwa kazi za uandishi za Robertson ni kitabu kilichokuja kuwa maarufu sana miaka ya 1913 na kuendelea,kitabu hiki kinaitwa Futility ambayo ilitoka mwaka 1898 ambayo haikuvuta sana watu hadi baada ya ajali ya Titanic mwaka 1912.Robertson alifariki mwaka 1915 katika chumba cha hoteli iliyokuwa ikijulikana kama Altlantic City hotel.

Robertson,katika hadithi yake hii ambayo ilijulikana pia kama "the wreck of the Titan" alikuwa akiizungumzia meli moja iliyokuwa ikijulikana kama Titan iliyokuwa ikifanya safarizake kutoka Southampton kwenda New York Marekani.Meli hii ambayo ilikuwa na sifa nyingi tu kuwa ni meli ambayo haikuwa na sifa ya kuzama ilipata ajali yake katika siku ya kwanza tu ya safari zake kwa kugonga barafu iliyokuwa ikielea katika bahari ya Altlantic......

Robertson anaendelea kusimulia kuwa Meli hiyo ilikuwa na uwezo wa kubeba watu 3000 na abiria waliokufa kwenye ajali hiyo ya kwenye meli ya hadithi walikuwa ni zaidi ya 1500.Titan,meli ya kwenye hadithi ya kijana huyu ilikuwa na urefu wa mita 800.Titan ilikuwa na majaketi maalum kwaajili ya kuogelea 24.Meli hii ilipata ajali mwezi April.Muda ambao ilipata ajali ni karibia na usiku wa manane...


Meli hiyo ya Titan ilipata ajali ikiwa katika eneo la kaskazini mwa Newfoundland katika bahari ya Atlantic kilomita zaidi ya 400 kutokea ianze safari zake na ilikuwa ikitokea Southamtpton U.K....

Meli hii ya Titan ilizama kwa kuanzia nyuma kisha ikakatika katikati na baadaye kuzama na watu wengi walipoteza maisha kutokana na baridi kali ya eneo hilo.....

Hiyo ikawa ndiyo safari ya kwanza na ya mwisho ya meli ya kwenye hadithi ya Robertson iliyojulikana kama Titan.

titanic

Kitabu cha hadithi cha Morgan Robertson maarufu kama "The Wreck of the Titan au Futility"

Ni hivyo kwa ufupi kuhusu hadithi ya kijana huyo aliyekuja kuwa maarufu baada ya kifo chake na hadithi hii...

Kuna mambo mengi tu yamefanana baina ya hadithi hii na tukio halisi la ajali mbaya kabisa ya Titanic....

Hapa chini ni baadhi ya mifanano baina ya Titan ya hadithi na Titanic halisi...

Meli zote zilipata ajali aneo moja na sababu ni moja,zilipata ajali eneo la kaskazini mwa Newfoundland na ziligonga barafu iliyokuwa inaelea katika bahari ya atlantiki...

Meli zote zilikuwa na sifa ya "meli zisizoweza kuzama"
Meli zote zilikuwa na upungufu wa makoti ya kuogelea...
Meli zote zilipata ajali umbali ule ule tokea zianze safari yake...
Meli zote majina yanafanana,Titan na Titanic...
Meli zote mbili zilikuwa na urefu unaofanana
Meli zote mbili zilipata ajali muda ule ule...
Meli zote zilikuwa zinatokea nchi ile ile,England...
Meli zote zilikuwa na uwezo unofanana wa kubeba abiria...
Meli zote zilipoteza maisha ya watu kwa idadi inayokaribiana....


Inawezekana ndiyo unasoma jambo hili leo kwa mara ya kwanza,wakati nilipokutana na tukio hili nilijiuliza mambo mengi sana kabla ya kuishia tu kushangaa na inawezekana na wewe ukajiuliza hivyo hivyo pia lakini utaishia kujiuliza tu na majibu yanaweza kuwa magumu sana kupatikana..

Inawezekanaje hadithi iliyoandikwa na mtu tu miaka 14 iliyopita ije kushabihiana kwa kiwango cha ajabu hivi na tukio la kweli? Kwanini?

Hii siyo kawaida.Hili ni miongoni mwa matukio mengi sana ya kustaajabisha yaliyowahi kutokea hapa duniani ambayo hayana majibu ya kuridhisha.Matukio yapo mengi sana lakini yanapuuzwa tu sijui ni kwanini....

Tumia wakati wako kujiuliza kuhusu hili halafu utajiambia wewe mwenyewe kama tupo kqwenye dunia salama kama tunavyofikiri....

No comments:

Post a Comment