Breaking

Thursday, November 22, 2018

KUMBUKUMBU:Agent Garbo 'Double agent' aliyesaidia kumwangusha Hitler

.com/
Habari zenu wakuu:

Ninapenda kuwasilisha historia fupi ya 'double agent' Juan Pujol Garcia almaarufu 'Agent Garbo' au Alaric Arabel.

AGENT GARBO NI NANI?

Garbo ni mzaliwa wa Spain(Barcelona) katika familia ya kawaida kabisa.Akiwa na umri wa miaka saba alipelekwa shule ya bweni ambapo alisoma kwa miaka minne kabla ya kuhamishiwa shule nyingine ambapo alikaa kwa miaka mitatu tuu na kuamua kuacha shule baada ya kugombana na mwalimu.Baada ya hapo alianza kusaidia kazi katika duka la vifaa vya ujenzi na baadae alisomea ufugaji wanyama na kufanya ufugaji wa kuku pamoja na biashara nyinginezo kama cinema na hotel ila hakupata maendeleo/faida.

.0/c_limit,w_740/fl_lossy,q_auto/v1493052977/articles/2011/11/27/garbo-the-spy-documentary-on-the-double-agent-who-helped-defeat-hitler/

Mnamo mwaka 1931, Garbo alipitia mafunzo ya kijeshi ya miezi sita ambayo yalikua ni ya lazima kwa wakazi wote.Garbo hakuyapenda mafunzo ya kijeshi na alikua akidai kuwa hawezi na hana sifa za kuwa mwanajeshi.Mwaka 1936, wakati Garbo akifanya kilimo cha ufugaji kuku, vilianza vita vya wenyewe kwa wenyewe.Jeshi la 'republicans' lilimwomba Garbo awe upande wao ila alikataa kwasababu baadhi ya ndugu zake walishakamatwa na hao "republican forces" na kufungwa kwa kosa la kutokua wazalendo.Garbo alijificha kwa 'girl-friend' wake hadi alipokamatwa na polisi na kufungwa kwa wiki moja.Baada ya kifungo alitengeneza kitambulisho cha kugushi kilichomwonesha hana umri unaofaa kulitumikia jeshi lengo likiwa kukimbia kulitumikia jeshi.

Licha ya kuwa awali alikwishakataa kujiunga na jeshi la republicans, agent Garbo alifanikiwa kujiunga na jeshi la 'republicans' kwa kutumia kitambulisho cha kugushi na baadae akafanikiwa kuhamia upande pinzani.Katika vita hii Garbo anajisifia kwa kutokutumia risasi hata moja kwa 'republicans' na kwa 'nationalists'.Akiwa katika kambi ya nationalists Garbo aliadhibiwa(kifungo) baada ya kuonesha huruma kwa adui yao.Baada ya kutoka kifungoni, Garbo alikutana na msichana ambaye baadaye walifunga ndoa na kupata mtoto mmoja.Kwa kifupi, Garbo hakufurahishwa na pande zote mbili za vita ambazo alizitumikia na hii ilisababisha kuwachukia zaidi 'Nazi Germany' na 'Sovietic union'.

Kutokana na Garbo kutowapenda wanazi, aliamua kuanzisha vita yake binafsi na Hitler kwa kutumia ushushushu, 'espionnage'.Uamuzi huu wa Garbo ulikua ni mgumu kwani hakuwahi kupitia mafunzo yoyote ya ushushushu na hakua na contacts za watu wowote ambao wangeweza kumsaidia.Akiwa na mke wake, Garbo alienda katika ubalozi wa uingereza uliokuwepo Madrid akiomba kujitolea kulitumikia jeshi la pamoja 'Allied' ila maombi yao yalikataliwa mara nne mfululizo.

Baada ya kukataliwa na ubalozi wa Uingereza, Garbo ilibidi ajaribu kupitia ubalozi wa ujerumani kwa kujifanya kuwa yeye ni m'nazi' na anaweza kuwasaidia katika kitengo cha ushushushu.Lengo lilikua ni lile lile la kupambana na Hitler 'from the inside'.Katika ubalozi wa Ujerumani alikutana na afisa aliyekua akiwasimamia maspy wakinazi aliyeitwa Federico.Akiwa na Federico, Garbo alimwadisia habari za kutunga zilizohusisha watu/contacts ambazo Garbo alikua nazo katika maeneo nyeti ya vita vya pili vya dunia na ili kumshawishi Federico Garbo alifanya safari ya Lisbon ambapo tayari vita ilikua imechanganya na watu wanapakimbia.

Akiwa Lisbon, Garbo alijichanganya katika kundi la waportugal waliokua wanahaha wakitaka kuikimbia nchi yao kutokana na vita.Baada ya kuwepo Lisbon kwa siku kadhaa, alifanikiwa kukutana na muispaniola mwenzake ambaye alikua na viza maalumu ya kidiplomasia ambayo ingemruhusu kusafiri bila shida.Garbo alitengeneza urafiki wa karibu na baadaye wakiwa katika mgahawa alifanikiwa kumhadaa na kwenda kuingia chumbani kwake ambapo aliipiga viza ile picha.Baadae aliitumia picha ile kujitengenezea viza ya kugushi akiwa hapo hapo Lisbon.Federico alibahatika kuiona ile viza na ndipo alipomuamini Garbo na kumwona atakua tunu katika kitengo chao na baadaye Garbo alichukuliwa rasmi na Abwehr, kitengo cha intelijensia cha Ujerumani.Hapa ndipo alipofundishwa mbinu za kutumia kuwasiliana kwani hakua amesomea ushushushu kabla.Pamoja na kozi fupi, alipewa wino wa kuandikia, kalamu, pesa za matumizi n.k

Baada ya kuajiriwa na Abwehr, Garbo alianza kazi rasmi akiwa Lisbon licha ya kuwa aliwadanganya wajerumani kuwa yupo Uingereza.Aliwapa taarifa za kipelelezi ambazo alikua akizibuni(taarifa za kufikirika).Katika taarifa hizi za kufirika Garbo aliwapa wajerumani taarifa za silaha za waingereza, maeneo ya kambi za kijeshi, safari za wanajeshi na misafara ya kijeshi kuelekea Malta n.k.Taarifa hizi alizichakachua kwa kutumia filamu za propaganda, vitabu vya simu, miongozo ya watalii, ratiba za treni na majarida mbalimbali.Licha ya kuwa taarifa hizi zilikua ni za uongo, ziliaminika kutokana na namna zilivyoandikwa kwa mtiririko wa matukio ambayo ilikua ni ngumu kuyatilia mashaka huku akitumia mtandao wa maagent wengine fake ambao alidai ni contacts zake katika baadhi ya miji.Katika taarifa zake, Garbo alikua akitengeneza matukio ya kuonyesha namna baadhi ya maagent fake walivyosababisha baadhi ya missions zake kufeli na hata pale wajerumani walipotilia shaka baadhi ya taarifa Garbo aliwasingizia hao maagent fake kwa ustadi wa hali ya juu na kujiweka katika upande wa kuzidi kuaminiwa.Katika kutekeleza hili ilifikia wakati akawa anatoa taarifa za kuuliwa kwa baadhi ya wasaidizi wake(fake) au kuumwa hali iliyosababisha Garbo kushindwa kutekeleza baadhi ya mission.Wachambuzi wa uingereza waliokuja kusoma taarifa hizi baadae, hawakuamini kuwa Garbo hakuwahi kufika uingereza wakati akiandika taarifa hizo.

.com/

Baada ya mda waingereza waligundua kuwa kuna mtu anawapa wajerumani taarifa za uongo.Hii ilikua baada ya Uingereza kuona nguvu kubwa iliyotumiwa na jeshi la Ujerumani kujaribu kuvizia msafara wa jeshi la uingereza ambao haukuwepo.Februari 1942, Pujol (au mke wake) alifanikiwa kuongea na afisa wa jeshi la marekani, Luteni Patrick Demorest ambaye alitambua kipaji cha Pujol(Garbo).Patrick alizungumza na wenzake wauingereza na ndipo Garbo alipohamia uingereza na kupokelewa na MI6 kabla ya kuhamishiwa MI5 mwezi Aprili 1942.Hapa ndipo Garbo alipokua 'Double agent' rasmi.

Akiwa Uingereza baada ya kupokelewa na MI6, alipohojiwa kuwa ni kwanini anapigana against Hitler;kama ilivyokua kawaida yake Garbo alitunga hadithi iliyomhusisha kaka yake wa kubuni aliyekua anaishi Ufaransa na ambaye aliuliwa na majeshi ya Hitler kwa kifo cha kinyama.Baada ya mahojiano ya kuhakikisha kuwa Garbo ni mtu salama, alikabidhiwa kwa afisa Tomas Harris(mwenye asili ya Spain kama Garbo) aliyekua MI5 ili amsimamie Garbo na kumpa maelezo ya kazi.

Harris na Garbo wakiwa MI5 waliendeleza kazi aliyokua ameianza Garbo na waliendeleza ule mtandao wa fake agents.Kilichoongezeka saivi ni kwamba walituma mtu katika miji yote yenye fake agents kwa ajili ya kukagua hotel na makasino ambayo yalikua yakitumiwa na hawa fake agents kwa lengo la kuweza kuelezea maeneo hayo kama yalivyo licha ya kuwa maagent wanaoishi humo ni wa kufikirika.Garbo na Harris walifanikiwa kutuma barua 315 kwenda Lisbon kwenye anuani waliyopewa na wajerumani na kutokana na taarifa za Garbo, ujerumani ilimrank Garbo kama spy wao namba moja kwa ubora ambaye baadaye walimtunuku 'the iron cross'.Pia mtandao feki wa Garbo uliwaimpress wajerumani hadi wakaona hamna sababu ya kuajiri maspy wengine Uingereza, Garbo anawatosha.Garbo alifanikisha yote haya kwa kuwapa taarifa za uongo kwa asilimia kubwa au taarifa za ukweli usiokua na athari kwa waingereza.Pia wakati mwingine alituma taarifa za kweli na zilizokua za hatari kwa waingereza lakini alihakikisha zinafika kwa kuchelewa ili hatari yake isiwe hatari tena.

Ukiachana na wajerumani, hata waingereza(na jeshi la pamoja kiujumla) walifurahishwa na kazi za Garbo.Ilipofikia siku ya kumu-attack Hitler Ufaransa(the D-day) kupitia operesheni iliyobatizwa 'Operation overload', Garbo alipewa kazi ya kulirubuni jeshi la Hitler juu ya eneo ambalo uvamizi utaingilia.Uvamizi ulipangwa kufanyiwa Normandy na Pujol(Garbo) alipewa kazi ya kuliaminisha jeshi la Hitler kuwa uvamizi hautafanyikia Normandy bali Pas de Calais, Ufaransa.Hii mission ya Garbo ilipewa jina la 'Operation fortitude'.

'Operation fortitude' ilifanikiwa kwa kutengeneza kambi kubwa ya jeshi kwa kutumia midoli ambayo iliwakilisha magari ya kivita, shehena za mafuta, viwanja vya ndege n.k Kambi hii ilikua imewekwa karibu na pwani ambayo haikua mbali sana na pas de calais, eneo ambalo Pujol alikua ana kazi ya kuwaaminisha wajerumani kuwa jeshi la mwingereza na mmarekani litaingilia hapo.Baada ya kutengeneza kambi ya midoli, Pujol aliendelea kuwaaminisha wajerumani kuwa uvamizi utafanyikia Pas de calais na hata mashambulizi yalipoanza Normandy aliwadanganya kuwa ilikua ni geresha tuu na kuwa mashambulizi yenyewe yamepangwa kufanyikia Pas de calais.Hii ilisababisha Ujerumani kuacha sehemu kubwa ya vikosi vyake Pas de calais na baadae Hitler kutolewa Ufaransa na kushindwa vita.
.844114/


Baada ya vita aliachana na mkewe na baadae kwa kushirikiana na MI5 alisafiri hadi Angola ambapo baadae walidanganya kuwa amefariki kwa ugonjwa wa Malaria na kisha akabadili utambulisho wake na kwenda kuishi Venezuella ambapo alikua anauza vitabu na zawadi katika duka dogo.Pujol alifariki mwaka 1988.

No comments:

Post a Comment