Breaking

Monday, January 27, 2020

Faida zitokanazo na kumsamehe yule aliyekukosea

Ni vema kuanzia sasa kuamua kubadilika kwa kuhakikisha kwamba hubebi vinyongo vya aina yeyote ile ndani mwako. Unapaswa kusamehe wale wote wanaokukosea kwa sababu:

Msamaha ni kuondoa uchungu wote ulioumbika ndani ya moyo wako kwa hiari yako mwenyewe.

Hivyo, unaposamehe unarudisha uhusiano wa awali uliovunjika. Msamaha sio wa mwisho wa mwaka jamani, msamaha ni tunu ya kila siku kwa maana hujui siku ya kufa kwako.

Tunaposamehe ndugu zangu tunajenga afya njema. Hii ni kwasababu, Uponyaji wa kweli huanzia moyoni. Kama mtu anasamehe kutoka moyoni basi huo ni msamaha wa kweli.

Watu hawataki kusamehe ndio maana wengine afya zao ni dhaifu. Uchungu ulio umbika ndani ya moyo una endelea kuwa tafuna.
Nasaha, "Usizeeke kabla ya wakati kwa ajili ya kuto kusamehe watu wengine".

No comments:

Post a Comment