Breaking

Sunday, January 12, 2020

HISTORIA YA ADOLF HITLER KUZALIWA MPAKA KIFO CHAKE

ADOLF HITLER Alikuwa dikteta wa Ujerumani kuanzia mwaka 1933 hadi kifo chake. ADOLF HITLER AKIWA MTOTO
Alizaliwa nchini Austria katika mji wa Braunau am Inn karibu kabisa na mpaka kati ya Ujerumani na Australia 20,april 1889 katika familia ya Alois Hitler na Clara Hitler,Alois Hitler ambaye ni baba yake Hitler [1837-1903] alikuwa ni mtoto haramu wa Maria Anna schicklgruber. mnamo mwaka 1842 Maria Anna aliolewa na Johann George Hiedler, baada ya kifo cha mama yake[1847]na baba yake wa kufikia ambaye ni Johann Hieldler [1856] Alois Hitler aliendelea kukua katika familia ya ndugu wa Johann aliyeitwa [Johann Nepomuk Hiedler. mwaka 1876 alihalalishwa na viongozi wa dini kuwa ni mtoto halali wa Johann Nepomuk Hiedler na akapewa jina jipya la George Hitler ambapo maana ya HITLER ni mtu aliyeishi ndani ya nyumba. Kuhusu baba yake halisi wa George Hitler bado ni kitendawili kwa kuwa inasemekana kuwa mama yake Maria Anna alikuwa ni mtumishi wa ndani katika familia ya KIJEWISHI, na kijana wa miaka 19 aliyeitwa Leopold Franknberger katika familia hiyo alimbaka Maria na kuzaliwa Alois Hitler na ndio sababu akaitwa mtoto haramu, hata hivyo taarifa za kuaminika juu ya Leopold bado hazijapatikana HISTORIA ADOLF HITLER Adolf Hitler alikuwa mtoto wa sita katika familia ya Alois Hitler na Clara Polz japo MAMA YAKE HITLER CLARA HITLER
kaka zake na dada zake wote walikufa wangali wachanga akiwa na umri wa miaka sita familia yake ilihamia Passau huko ujerumani na baadaye tena 1894 ikahamia leonding hata hivyo mwaka 1895 Alois alistaafu kazi yake huko Hafeld ambako akawa mkulima na mfugaji wa nyuki. Shughuli za kilimo na ufugaji zilifeli vibaya sana na familia ya hitler ililazimika kuhamia Lambach, Hitler alianza kujifunza kuimba nyimbo za dini kanisani na alidhamiria kuwa muhubiri, mwaka 1898 familia yake ilihamia makazi ya kudumu LEONDING, NYUMBA ALIYOISHI ADOLFU HITLER AKIWA HUKO LEONDING
Mnamo mwaka 1900 mdogo wake Hitler Edmund alikufa kwa ugonjwa wa SURUA kifo ambacho kilimuathiri sana jambo lililopelekea Hitler kubadilika kitabia kwa sehemu kubwa akawa mbishi, mtundu na akadiliki kupigana na baba yake na walimu wake tofauti na awali ambapo alikuwa ni mtoto mtiifu na mwelewa, baba yake alipata mafanikio makubwa katika shughuli za usimamizi wa mila na desturi[chifu] jambo amabalo alitaka mwanaye Adolf Hitler afuate nyayo zake jambo ambalo lilipingwa vikali na mwanae ambaye alitaka apelekwe kwenye shule ya sanaa hii ilipelekea kutokea tofauti kubwa kati yao. Mwaka 1900 Alois Hitler alimpelekea mwanae katika shule ya secondari iliyojulikana kwa jina la REALSCHULE ambapo hitler alikubali kwa shingo upande na akafeli vibaya sana ktk mitihani yake hii alifanya makusudi kwa kujua kuwa baba yake akiona maendeleo yake mabovu shuleni angebadili uamuzi wake na kumpeleka mwanae katika shule ambayo ni ndoto yake[sanaa] na hivyo kushindwa kuendelea na masomo kama vijana wengi wa kijerumani, Hitler alianza kushika asili na desturi za kijerumani ambazo kwa kipindi hicho ilikuwa ni ya kibaguzi, Hitler na marafiki zake walianza kutumia salamu ya kijerumani[HEIL] na kuimba nyimbo za kijerumani badala ya zile za AUSTRALIA, Baada ya kifo cha baba yake kilichotokea 3,january/1903 maendeleo ya kitaaluma kwa Hitler yaliendelea kuzorota kwa kasi na baadaye mama yake alimuondoa kwenye shule hiyo Kutoka mwaka 1905 Hitler aliishi na mama yake yakiwa maisha mapya baada ya baba yake kufariki, mwanzo alifanya kazi ndogondogo na baadaye akawa anafanya kazi za upakaji rangi ikiwa ni pamoja na kuchora, kuuza rangi za maji nk. MOJA YA MAJENGO YALIYOPAKWA RANGI ZA MAJI NA ADOLF HITLER ENZI ZA UHAI WAKE
alidhamiria kuendeleza kipaji chake cha sanaa kwa kuomba kujiunga na chuo cha VIENNA,S ACADEMY OF FINE ART lakini alikataliwa kwa mara ya kwanza 1907 na baadaye akakataliwa tena 1908, kiongozi wa chuo alitoa maoni kuwa Hitler alikuwa na uwezo mkubwa katika uchoraji lakini hakuwa na sifa za kitaaluma yenye ushahidi kwakuwa hakuwa na cheti cha kuhitimu elimu ya secondari. Mnamo 21/12/1907 mama yake Clara Hitler akiwa na umri wa miaka 47 alifariki kwa ugonjwa wa kansa ya titi, kifo cha mama yake kilisababisha mfumo wa maisha yake kuyumba na kulazimika kupoteza lengo la kusoma kichwani mwake na akaanza maisha mapya kwa kutafuta kazi za vibarua kwa ajili ya kujikimu, maisha hayo yalifanya kuwa mtoto wa mitaani asiye na pa kukaa. Kwa muda ambao Hitler alikuwepo VIENNA kulikuwa na chuki za kidini pamoja na ubaguzi wa rangi, hofu ya kuchukuliwa kama mkimbizi kutoka mashariki ilitwala na kuenea kwa kasi. Hitler alipendelea kusoma magazeti ya DEUSCHES VOLKBLATT ambayo yalivumisha chuki kwa wakristo ambapo hitler alikuwa ni mmoja wao Mei,1913 Hitler alikabidhiwa shamba lake ambalo lilikuwa ni urithi wa marehemu baba yake na alihamia MUNICH kukwepa kujiunga na jeshi la Australia hii ni kwasababu jeshi hilo lilikuwa na mchanganyiko wa jamii tofautitofauti jambo ambalo hakulipenda Hitler. Katika VITA YA KWANZA YA DUNIA, Hitler alikuwa akiishi MUNICH na alijitolea kulisaidia jeshi la BAVARIA akiwa kama ni mwananchi wa Australia na aliwekwa kwenye kikundi cha RESERVE INFANTRY REGIMENT namba 16 combania namba 1 HITLER NA RAFIKI ZAKE WA KIKOSI CHA RESERVE INFANTRY REGIMENT
na alikuwa kama mpeleka taarifa kikosi cha magharibi ya mbele Ufaransa na Ubelgiji na muda wote alikuwa nyuma ya mstari wa kikosi kilichokuwa mbele ya mapigano vikosi alivyotumikia wakati huo ni kikosi cha YPRES, SOMME, ARRAS na PSSCHENDAELE na alijeruhiwa bega la kulia alipokuwa SOMME. Alifanya kazi kwa juhudi kubwa na baadaye akatunukiwa nishani ya msalaba wa chuma na akapanda cheo kuwa PRIVATE, mwaka 1918 Kwa amri ya Lieutenant Hugo Gutmann, Hitler alitunukiwa nishani ya chuma daraja la kwanza na kupandishwa cheo kuwa COPLO. KUINGIA SIASA Baada ya vita alikosa kazi lakini aligundua kipawa chake cha kuhutubia watu, akajiunga na siasa na kuingia katika chama kidogo cha Nazi alikopanda ngazi haraka. KADI YA HITLER YA CHAMA CHA DAP
JARIBIO LA MAPINDUZI Hitler alivutwa sana na mfano wa Benito Mussolini kiongozi wa kifashisti wa Italia aliyefaulu mwaka 1922 kupindua serikali ya Italia kwa maandamano makubwa ya wafuasi wake kuelekea Roma Mwaka 1923 Hitler alijaribu kumwiga Mussolini kwa kupindua serikali ya Bavaria - kama utangulizi wa kupindua serikali ya kitaifa huko Berlin - lakini alikamatwa na kuhukumiwa kwa uasi huo kifungo cha miaka mitano, ingawa alitumikia miezi tisa tu. Chama chake kilipigwa marufuku. BENITO MUSSOLIN WAKIWA NA ADOLF HITLER KWENYE MKUTANO WA HADHARA
Hitler akiwa kijana aliwahi kusoma vitabu vya Mwingereza Chamberlain aliyedai kwamba kuna aina mbalimbali za watu wenye tabia na thamani tofauti sana. Akiwa gerezani aliandika kitabu kilichoitwa "Mein Kampf("Mapambano Yangu") alikojaribu kueleza imani na siasa zake. Humo alieleza pia chuki dhidi ya Wayahudi na itikadi yake ya ubaguzi wa kimbari. Katika itikadi hiyo mbari ya juu ni watu wa Ulaya ya Kaskazini aliowaita "Waaria na wale ambao ni duni zaidi ni watu weusi. Vikundi vingine vimo katikati. Lakini watu wabaya kabisa katika itikadi hiyo ni Wayahudi ambao ni wajanja wakuu upande mmoja, lakini hawana uwezo wa kuunda kitu kwa upande mwingine. Hivyo wanajaribu kwa ujanja wao kutawala dunia kwa kuiba fikra na mafanikio ya Waaria. Kujenga chama Baada ya kutoka gerezani alirudia siasa. Alijitahidi kushika utawala wa chama cha NSDAP akakubaliwa kuwa kiongozi mkuu. Ndani ya chama alianzisha vikosi viwili vilivyovaa sare vikifanya mazoezi kama wanamgambo na kuwa tayari kupigana na maadui wa kisiasa wakati wa maandamano. Kikundi cha SA ("Sturmabteilung" - "Kikosi cha kushambulia") kilikuwa na watu wengi sana kikavuta hasa wanaume wasio na kazi waliovaa sare ya kahawia Kikosi cha pili kilikuwa na watu wachache kikaitwa "SS " ("Schutzstaffel" - "Kikosi cha ulinzi") waliovaa sare nyeusi. Chama chake hakikufaulu hadi 1929 , wakati uchumi wa dunia pamoja na wa Ujerumani ulipoporomoka vibaya katika mdodoro mkuu Mamilioni waliachishwa kazi na kuona njaa . Katika hali hiyo watu walianza kupigia kura vyama vyenye itikadi kali. Katika uchaguzi wa mwaka 1930 kura za NSDAP ziliongezeka kutoka 2.6% hadi 18.3%. Serikali za Ujerumani zilikuwa za vyama vingi na dhaifu. Mwaka 1932 chama cha NSDAP kilipata 33% za kura na kuwa chama chenye kura nyingi zaidi nchini na chama kikubwa katika bunge . Katika hali hiyo viongozi wa Dola la Ujerumani waliamua kumwingiza Hitler katika serikali mwaka 1933. Chansela na kiongozi wa Ujerumani Tarehe 30 Januari Hitler akawa Chansela wa Ujerumani. Mara moja alichukua nafasi kuwakandamiza wapinzani wake na baada ya mwaka mmoja hata wale waliomwingiza madarakani. Baada ya mwaka mmoja utawala wake ulisimama imara kabisa ilhali wapinzani wengi walikamatwa na kupelekwa katika makambi ya KZ Hitler alifuata siasa ya kujenga uchumi na kurudisha watu kazini akibahatika kwamba uchumi wa dunia ukapaa tena. ADOLF HITLER MUDA MFUPI BAADA YA KUAPISHWA KAMA KANSELA WA UJERUMANI
Hitler alifuta mapatano yote ya Ujerumani yaliyoweka mipaka kwa ukubwa wa jeshi lake kuwa watu 100,000 tu akajenga jeshi kubwa zaidi, akaanzisha utawala wa kidikteta wa "Dola la Tatu akipiga marufuku vyama vya upinzani . Alitesa wapinzani wote na watu wa mbari alizochukia, hasa Wayahudi Siasa dhidi ya Wayahudi Chuki dhidi yaWajerumani waliokuwa Wayahudi aliionyesha kwa sheria mbalimbali zilizokuwa kali zaidi na zaidi. Idadi ya Wayahudi katika Ujerumani ilikuwa ndogo, takriban nusu milioni kati ya wakazi milion62. Kila Mjerumani akitaka kuajiriwa na serikali au kupata nafasi ya masomo alitakiwa kuorodhesha wazazi na mababu hadi kizazi cha pili. Kwanjia hiyo Hitler alipanga Wajerumani wote katika vikundi vya "Waaria (ambao hawana Wayahudi katika familia), "Wayahudi" (watu wenye asili ya Kiyahudi, hata kama wameshakuwa Wakristo tangu vizazi kadhaa au hawakufuata dini "Wayahudi nusu" kama mzazimmoja alikuwa Myahudi, "Wayahudi robo" kama mmoja kati ya mababu na mabibi wanne alikuwa Myahudi. Wayahudi na Wayahudi nusu walifukuzwakatika ajira ya serikali na walikataliwa kufanya kazi mbalimbali. MAITI ZA WAYAHUDI WALIOUAWA KWA AMRI YA ADOLF HITLER
AMRI YA KUWACHOMA MOTO WAYAHUDI ILIYOSAINIWA NA ADOLF HITLER SEPT 1 1939
Sheria kuhusu "Aibu wa mbari" ilikataza ndoa kati ya "Waaria" na "Wayahudi"; "Wayahudi" waliondolewa uraia kamili. Tokeo moja la siasa hiyo lilikuwa kuondoka kwa Wayahudi wengi kidogo katika Ujerumani; baada ya mashambulizi makali na mauaji mwaka 1938 mwelekeo huo uliongezeka. Hasa wanasayansi na wasanii wengi walihamia nchi huru. Siasa yake katika mwaka 1939 ilisababisha Vita Kuu ya Pili ya Dunia Hitler alifuata mwanzoni siasa ya kukusanya Wajerumani wote wa Ulaya katika Dola la Ujerumani. Mwaka 1938 alifaulu kuteka Austria na maeneo ya Wajerumani katika Ucheki bila upingamizi wa kimataifa. Lakini aliposhambulia Poland tarehe 1 Septemba tendo hili lilikuwa mwanzo wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia kwa sababu Uingereza walisimama imara kwa mikataba ya kusaidiana na Poland. Wakati wa vita Hitler alichukua mwenyewe uongozi mkuu wa jeshi. Mwanzoni alifaulu hata dhidi ya ushauri ya majenerali wake, hasa wakati wa vita dhidi ya Poland na Ufaransa. Lakini maazimio yake ya 1941 ya kushambulia Urusi na kutangaza hali ya vita dhidi ya Marekani yalikuwa mwanzo wa mwisho wake. Nguvu ya kiuchumi wa Ujerumani haikutosha kushindana na dunia yote. Wakati wa vita aliamuru uuaji wa Wayahudi wote wa Ulaya na inakadiriwa alifaulu kuwaua takriban milioni sita (2/3 ya Wayahudi wote wa Ulaya) pamoja na watu vya mbari mbalimbali kama Wasinti (kati ya 200,000 na 1,500,000). Hasa alipoona ya kwamba vita dhidi ya Urusi haikufaulu haraka jinsi alivyotegemea aliamua kumaliza jambo lililosababisha chuki yake hasa. Azimio la "usuluhisho wa mwisho wa suala la Kiyahudi" lilichukuliwa mwisho wa mwaka 1941 na kutangazwa mbele ya viongozi wachache mnamo Januari 1942 katika Mkutano wa Wannsee Baadaye siasa ya kuwatenda Wayahudi vibaya na kuwaua katika maeneo fulani ilibadilishwa kulenga Wayahudi wote katika nchi zote zilizokuwa chini ya athira ya Ujerumani au kutekwa na jeshi lake. Hadi mwisho wa vita Wayahudi walikusanywa kutoka kote Ulaya na kupelekwa kwa reli hadi makambi ya mauti Mwisho wa vita na kifo Maafisa wa jeshi ya Ujerumani walipanga mara kadhaa kumwua Hitler lakini hawakufanikiwa.Tarehe 20 Julai alijeruhiwa na bomu ya Stauffenberglakini hakuuawa. Mwishoni mwa vita Hitler alikaa Berlin hadi jeshi la Kirusi lilipokuwa limeshaingia mjini. Tarehe 30 Aprili alijiua kwa sumu pamoja na mpenzi wake Eva (alimwoa masaa tu kabla ya kujiua) na mbwa wake mpendwa "Blondi Maiti zilichomwa kwa petroli lakini zilitambuliwa na Warusi kutokana na meno yake. ADOLF HITLER AKIWA NA MKEWE PAMOJA NA MBWA WAKE ALIYEMPENDA SANA NA AMBAYE WALIKUFA PAMOJA.

No comments:

Post a Comment