Breaking

Wednesday, January 15, 2020

HISTORIA YA MISRI NA MATUKIO YA KALE

Kulitokea wataalamu mbalimbali waliojaribu kutoa nadharia ili kufafanua asili ya binadamu kuongoza wengine. Yaani walikuwa wakifafanua asili ya uongozi katika maisha ya binadamu. Yaani ilikuwaje mpaka binadamu akahitaji kuongozwa???. Wapo waliodai uongozi ulianzia katika familia na wapo waliodai kuwa uongozi ulianza sehemu ambazo watu walienda kuchota maji. Na mara baada ya kufahamu kwa uachache juu ya nadharia za uongozi ulivyokuwa na asili yake. Kwa nchi kama Misri suala la uongozi lilikuwa ni njambo muhimu sana na kiongozi alikuwa na nguvu sana. Viongozi wa Misri walifahamika kama Farao. Kulikuwa na mafarao wengi na kila mmoja alikuwa na uongozi wake na kila mmoja alikuwa na mfumo wake. Hivyo kabla ya nchi ya Misri ya juu (Ta-Shome) na Misri ya Chini (Ta- mehu) kuungana kwenye miaka ya 3100 na kuwa nch moja, bado kila nchi ilikuwa na farao wake. Lakini baadae kwenye miaka ya 3000 iliyopita nchi hiyo ilkuwa chini ya farao mmoja. Na mpaka kufikia miaka ya 2000 iliyopita kulikuwa na Farao aliyefahamika kwa jina la Amenenhet I. Farao huyu alijiwekea historia ya kuwa farao wa kwanza kuchagua farao mwingine atakayemrithi mara baada ya kufa au kumaliza muda wake katika uongozi. Ifahamike kuwa kabla ya hapo mfumo wa uongozi haukuwa wa kurithi, kila mtu mwenye sifa alipaswa kuwa farao. Lakini kuanzia miaka 2000 iliyopita, farao Amenenhet I alianzisha mfumo wa kuchagua farao atayemrithi. Kipindi cha miaka ya 2000 iliyopita, Misri ilifanikiwa kujenga miji mingi na kufanya biashara na nchi zingine zilizopata kuwepo kwenye miaka hiyo. Na pia ndio kipindi ambacho Wamisri walifanikiwa kujenga makaburi ambayo mafarao walikuwa wakizikwa na watu wengi waliokuwa wakichaguliwa. Na hii ilifanyika kwa kuwa waliamini kulikuwa na maisha baada ya kufa. Kwa hiyo huo ndio ukawa mwanzo wa mfumo wa kurithishana uongozi katika nchi za Misri kuanzia miaka ya 2000 iliyopita.

No comments:

Post a Comment