Breaking

Sunday, January 12, 2020

HISTORIA YA OSAMA BIN LADEN- SEHEMU YA PILI

KUANZISHWA KWA AL QAIDA Mwaka 1988 jeshi la Kisovyeti ilianza kuondoka Afghanistan. Viongozi wa mujahedin Waarabu katika Afghanistan waliokuwa Bin Laden na Wamisri kama Aiman az-Zawahiri na Abdullah Azzam walishauriana pamoja namna ganikuendeleza jitihadi zao. Walitofautiana kama kulenga serikali za nchi za Kiarabu zisizokuwa za kidini kama huko Misri au kuhamia Palestina au kupeleka jihadi yao kwenda jamhuri za Kisovyeti za Asia ya Kati kama Tajikistan zilizokaliwa na Waislamu.Mkutano huu ulifanyika katika kambi lililoitwa "al-qaida" kwa kiarabu. Hili lilikuwa baadaye jina kwa kundi lililoongozwa na bin Laden. Sehemu ya mujahidin Waarabu walimfuata bin Ladin katika kushambulia jeshi la serikali la Afghanistan iliyoendelea kujitetea hata baada ya kuondoka kwa Wasovyeti. Mwaka bin Laden alitembelea tena Saudia akashauriana na serikali kuendelea namna gani. Alipopewa jibu heri arudi kwake akatii akarudi pamoja na kikosi chake. Baada ya kurudi Saudia aliishi Madina na Jiddah akaingia tena katika kampuni ya familia yake na kusimamia miradi ya ujenzi wa barabara. Wengi walimtazama kama shujaa aliyewajibika kwa kiasi kikubwa kufukuza Umoja wa Kisovyeti kutoka Afghanistan. Mwaka 1990 serikali ya Saddam Hussein wa Irak ilivamia Kuwait. Serikali ya Kisaudi iliogopa mashamblio mengine dhidi ya Saudia ikakubali kufika kwa wanajeshi wa Marekani nchini. Osama aliona hatua hii kama marufuku kwa sababu aliamini Uarabuni ni nchi takatifu kutokana na mahali patakatifu pa Kiislamu pa Makka na Madina akajitolea kukusanya mujahidin 100,000 kama ulinzi dhidi ya Saddam badala ya kuwaruhusu Wamarekani.Lakini serikali ilikataa.Wanajeshi kadhaa wa Marekani waliendelea kukaa katika Saudia hata baada ya ushindi juu ya Irak katika vita Hapo bin Laden alianza kupinga waziwazi siasa ya serikali yake. Kutokana na ugomvi huu aliamua kuhamia nchi ya Sudan alipotumia utajiri wake kuanzisha miradi, mashamba na makampuni lakini pia makambi kwa ajili ya vijana wafusi wa Uislamu mkali waliomfuata na kuhamia Sudan. Alikaa karibu na viongozi wa kundi la Al-Jihad ya Misri waliowahi kushirikiana naye Afghanistan na kupambana dhidi ya serikali ya rais Mubarak. Kukaa kwa Wamarekani katika Saudia na kuingilia kwa Marekani katika vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia tangu Desemba 1992 kwa niaba ya Umoja wa Mataifa ilileta imani kati ya Waislamu wakali kuwa nchi za Magharibi wanaendesha vita ya misalaba mipya. Katika miaka iliyofuata yalitokea mashambulio mbalimbali dhidi ya wanajeshi na taasisi za Kimarekani yaliyoendeshwa na wanajihadi mbalimbali kama vile huko Yemen 1992 na shambulio la 1993 dhidi ya World Trade Center mjini New York. Haijulikani hadi leo ni kiasi gani ya kwamba Osama na Al Qaida yalioshiriki katika mipango hii lakini watendaji walikuwa watu wenye mawasiliano na Bin Laden. Pia alitoa pesa kwa vita ya harakati ya kijihadi ya Groupe Islamique Armee nchini Algeria na kuhubiri dhidi ya serikali ya Saudia. Hapo Saudia ilifuta uraia wake na kukamata mali yake nchini. Familia ya bin Laden ilitangaza ya kwamba walimfukuza katika ukoo. Mwaka 1995 wanajihadi wa Al-Jihad ya Misri walijaribu kumwua rais Mubarak wa Misri kwenye mkutano wa Umoja wa Muungano wa Afrika mjini Addis Ababa. Hapo Umoja wa Mataifa ilidai Sudan kuwakabidhi kwa mahakama watendaji waliotoka huko na kutangaza hatua dhidi ya taifa hili. Sudan ilijaribu kuepukana na kuadhibiwa na jumuiya ya kimataifa haikutaka kuonekana kama msaidzi wa ugaidi ikalazimisha wanajihadi wa kimataifa kuondoka. Tarehe 18 Mei 1996 Osama bin Laden alipelekwa tena Afghanistan. Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko la fatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram(msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu .. Kwa msada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri Za Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoMkuta" Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano. Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban Ahmad Shah Massoud kwa bomu. Tendo hili lilifuatwa na mashambulio ya kigaidi ya 11 Septemba 2001 katika Marekani yaliyoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Bora na kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo. JENGO LA BIASHARA LA KIMATAIFA LILILOLIPULIWA NA BOMU NA KIKUNDI CHA AL-QAIDA SEPT 11 2001
Jitihada Za Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti. Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad KIFO Osama bin laden aliuawa Pakistan mnamo may 2, 2011 na kikosi maalumu cha kijeshi toka Marekani kilicho- ongozwa na NEPTUNE SPEAR. Mpaka leo bado ni kitendawili juu ya chanzo hasa cha mgogoro mkubwa kati ya Osama bin Laden na Taifa la MAREKANI OSAMA BIN LADEN MUDA MFUPI BAADA YA KUUAWA NA WANAJESHI WA MAREKANI

No comments:

Post a Comment