Breaking

Wednesday, January 15, 2020

HISTORIA YA NCHI YA IRAN

[KUTOKA KATIKA MUENDELEZO WA MAKALA ZANGU JUU YA MATAIFA YALIYOKUWA HIMAYA ZA DUNIA HEGEMONY]
Na, Godfrey Godstar.
THURSDAY, 21/9/2017.
Hii inayoitwa “Dola himaya na miliki kuu ya ulimwengu” yani (World super-supremancy empire) “World Hegemony” inavyo fahamika katika msamiati katika kingereza ni nadharia ya dola moja kuongoza nyingine kisiasa, kiuchumi na kijeshi. Taifa moja linakuwa kiranja wa mataifa mengine duniani. Utaratibu huu ulikuwepo toka zama za kale pale ambapo mwanadamu alipo anza ustarabu wa maisha ya kijamii. Katika huu ulimwengu wa sasa dola za China, Urusi na Marekani ndiyo wanaopambana sasa hivi kujisimika ukuu wa Hegemony. Kila mmoja anataka awe kiranja wa dunia kiuchumi, kisiasa na kijeshi.
Mipango ya dola moja kuwa kiranja wa dunia haijaanza leo. Karibu Karne 7 Kabla ya Ujio wa Kalenda ya kawaida (B.C.E) dola kama Mesepotamia ya Nimrod I, Umed na Uajemi ya Mfalme Koreshi II , Ugiriki ya Kale ilitawaliwa na Alexander III of Macedon, kwa umaarufu zaidi alifahamika kama Alexander the Great, Rome ya Julius Caiser katika karne ya 1 kabla ya kuja kwa yesu pamoja na dola kama Uingereza katika miaka ya 600-1800 AD Ujerumani, USSR na hatimaye hii ya sasa ya USA. Taifa moja linakuwa na sera ya kutaka kutawala dunia. Wakuu wa mataifa mengine wawe wafuata maagizo. Taifa moja linakuwa na mipango endelevu ya kutawanya mabavu yake ya kijeshi duniani ili kumiliki uchumi wa dunia.
Unapokuwa na uchumi imara pamoja na uwezo mkubwa wa kijeshi, dunia utaielekeza upande wako. Na hapo ndipo kwenye vita kubwa ya katika ulimwegu huu •Labda tuanze upembuzi katika sehemu ya kwanza kabla atujaenda kuigusa dola ya uajemi yenyewe "Je Dola-Himaya na miliki kuu duniani (World Hegemony) ni nini? Kimsingi Ni Taifa kuu katika dunia na ambalo ndio Lina kuwa na nguvu kiuchumi, Kijeshi, Kisiasa, Kiushawishi, Kiutawala, Kiteknologia, Kimamlaka na Kijasusi. Hivyo unaposikia neno Hili utambue kuwa taifa lolote linapofikia nafasi hii kimsingi dunia nzima inakuwa chini ya himaya ya msukomo na ushawishi kutoka Dola hilo kuu. Toka dunia imeanza kuwa na usatarabu wa utawala wa kijamii kumekuwepo na "Dola-Himaya na miliki kuu (World Hegemony) 8 za dunia mpaka sasa ambazo ni zifuatazo kwa mtililiko wake....
1-Mesopotamia Empire. (Himaya ya Mesopotamia) . 2-Persian Empire (Himaya ya Uajemi). 3-Greece Empire (Himaya ya Ugiliki). 4-Rome Empire (Himaya ya Roman). 5-United Kingdom of Great Britain Himaya ya Uingereza). 6-Herman and Prussia Empire (Himaya ya Ujerumani). 7-Union Soviet Socialist Republic Empire ( Himaya ya USSR). 8-United States of America Empire (Himaya ya Marekani). Baada ya kutazama utangulizi huo sasa ni vyema tukareje kataka maudhui ya andiko hili juu ya kuifahamu dola ya uajemi/umedi kama dola himaya ya pili ya dunia baada ya kufanikisha kuangusha miliki ya Mesopotami na kuanza kujitanua kwa kuitawala dunia…… sasa twende kewnye upembuzi sasa…..
UTANGULIZI:
UMEDI NA UAJEMI/IRAN (PERSIA)
Dola ya Uajemi (Jina hilo linatokana na Kiarabu; العجم- al-'ajam; pia: Iran - ايران) ni nchi inayopatikana katika bala la Asia ya Magharibi. Ambayo kwa sasa inafahamika kama جمهوری اسلامی ايران (katika kiarabu) Jomhūrī-ye Eslāmī-ye Īrān au Jamhuri ya Kiislamu ya Uajemi. Kauli mbiu ya taifa hilo la Kiajemi ni “Esteqlāl, āzādī, jomhūrī-ye eslāmī” Yani ("Uhuru, Huria, Jamhuri ya Kiislamu") Wimbo wa taifa wa dola hilo hutambulika kama “Sorūd-e Mellī-e Īrān” Mji mkuu wake ni Tehran Unaopatikana katika 35°40′ N 44°26′ E, Katika taifa hilo Lugha rasmi Kiajemi (Farsi), Kiongozi Mkuu ni Ali Khamenei Na Rais wa sasa wa nchi hiyo ni Hassan Rouhani.
Dini kuu ya nchi hiyo ni Uislam Dhehebu ya Shia na utawala unao hudumu kwa sasa ulihatamu mamla ka yaliyotokana na Mapinduzi yaliyofanyika 11 Februari 1979. Ukubwa wa Eneo la taifa hilo kwa sasa ni 1,648,195 km² (na ya 18 kwa ukubwa katika bara la Asia), idadi ya watu katika nchi hiyo kwa takwimu za sense ya 2013 ni kadirio la 78,192,200 (pia ni ya ya 18kwa idadi ya watu Asia ) fedha yake hutabulika kwa jina la Rial (ريال) (IRR) na kodi ya simu ya taifa hilo ni +98.
Jina rasmi ya nchi ni Jamhuri ya Kiislamu ya Uajemi au Iran. Uajemi imejulikana tangu kale kama nchi iliyochangia mengi katika historia ya binadamu. Kwakuwa iliwahi kuwa miliki kuu ya dunia iliwahi kuwa taifa kubwa lenye nguvu na himaya iliyo tambaa mashaliki ya kati na ulaya ikiwa ni pamoja na ukanda wote wa dunia ya kale. Dola ya Irani Imepakana na Afghanistan, Armenia, Azerbaijan, Iraq, Pakistan, Uturuki na Turkmenistan. Upande wa kusini kuna mwambao wa Ghuba ya Uajemi (Bahari Hindi) na upande wa kaskazini ni mwambao wa Bahari ya Kaspi. Toka karene ya 16 Tehran ndio mji mkuu, pia ni mji mkubwa nchini ya Iran ya sasa.
Uajemi au Iran ya sasa umegawiwa kwa mikoa 31 inayoitwa "ostan" chini ya gavana anayeteuliwa na rais. Kila mkoa huwa na wilaya (shahrestan) na ngazi ya chini zaidi ni mitaa (bakhsh). Chini ya mitaa kuna kata (dehestan) zinazojumlisha vijiji kadhaa. Idadi ya Watu Iran ina mchanganyiko wa makabila na dini uliounganishwa na utamaduni na lugha ya Kiajemi, ambayo inatumiwa na wananchi walio wengi na ndiyo lugha rasmi, ikifuatwa na lugha nyingine za jamii ya Kihindi-Kiulaya, lakini pia za jamii nyingine kama Kiazeri (16%) na Kiarabu (2%).
Katika Dini Uajemi iliwahi kuwa na dini zake za Uzoroasta na Umani. Kuanzia karne ya 4 AD idadi ya Wakristo ilikua. Tangu karne ya 7 Waarabu Waislamu walivamia Uajemi na kuifanya polepole kuwa nchi ya Kiislamu. Katika karne ya 16 baada ya kutanuka kwa uislamu duniani Uislamu wa Kishia ulitangaziwa kuwa dini rasmi nchini. Leo hii takriban asilimia 90 za wakazi ni Waislamu Washia. Karibu 10% ni Wasunni, hasa katika maeneo karibu na mipaka; kiutamaduni Wasunni wengi ni Wakurdi, Wabaluchi au Waturkomani.
Wafuasi wa dini nyingine kwa jumla ni kama 1% ya wakazi wote. Kundi kubwa ni Bahai lakini dini yao ilipigwa marufuku baada ya mapinduzi ya Kiislamu. Kundi linalofuata ni Wakristo kati hao kundi kubwa ni Waarmenia, halafu Wakaldayo. Wayahudi wa Uajemi ni kundi kubwa kati ya nchi zote za Kiislamu wa mashariki ya kati (0.01%). Wazoroasta wamebaki pia (0.03%). Kundi dogo sana ni Wamandayo wanaoitwa pia wafuasi wa Yohane Mbatizaji. Labda sasa tulejee katika maudhui ya makala hii kwa kufanya upembuzi wa dola ya Uajemi na umedi kama taifa la pili kama dola himaya na miliki kuu ya ulimwengu.
HISTORIA YA UAJEMI NA UMMED
Dola hiyo tunayokwenda kuizungumzia katika historia yake ilianza toka Tangu mwaka 500 BC wakati huo kulikuwa na makabila madogo ya nchi yaliunganishwa, na hii ilikuwa mwanzo wa milki ya Uajemi ambayo baadae ilikuja kuwa miliki kuu na dola himaya kuu ya dunia ambayo ilichukuwa nafasi hiyo iliyotoka katika dola la MESOPOTAMIA . Tangu mwaka 500 BC makabila madogo ya nchi yaliunganishwa, na hii ilikuwa mwanzo wa milki ya Uajemi. Mfalme Koreshi II (CYRUS THE GREAT)aliunganisha Uajemi yote chini ya mamlaka yake akavamia sehemu za Uturuki ya leo na Babeli na kuunganisha nchi hizo. Pia huyu Koresh ll (Cyrus mkuu) pia ndie mwanzilishi wa Himaya na Dola kuu ya Umedi na Uajemi (Median and Persia) katika Uajemi ya kale hutazama kama baba wa taifa na mwasisi wa Himaya ya Uajemi.
Mfalme Koreshi II ndie mwenye historia ya kuijenga dola hilo kwani aliunganisha Uajemi yote chini ya mamlaka yake akavamia sehemu za Uturuki ya leo na Babeli na kuunganisha nchi hizo. Waandamizi wake walipanua milki hadi Misri, Uhindi na Ugiriki ambapo miliki hiyo ilifanya ustaarabu wake kuenea ulaya kuifanya eneo hilo kuwa eneo muhimu katika. Milki hiyo baadae ilikuja kuanguka na ilikwisha baada ya kushindwa na Aleksanda Mkuu kutoka dola ya Ugiliki lakini nasaba za Waparthia na Wasasanidi waliendelea kufufua milki ya Uajemi tena na tena
UAJEMI NA UMEDI YA KALE
Uajemi ya Kale ni kipindi katika historia ya Uajemi kilichotokea kabla ya kuingia cha Uislamu nchini hapa na hasa kipindi cha milki kubwa. Nasaba mbalimbali za watawala ziliunda madola makubwa yaliyounganisha nyanda za juu za Uajemi pamoja na nchi za jirani. Athira ya Uajemi ilikuwa kubwa mno katikdunia ya kale kwani ilitawala dunia na ilikuwa na nguvu iliyoogopewa kalibu dunia nzima katika nyakatizile. Dola hiyo ilihatamu nguvu na kuwa taifa ambalo ilikuwa nchi muhimu zaidi katika Asia ya Magharibi ambayo dunia ya wakati huo kwa karne nyingi. Tangu mwaka 500 BC makabila madogo ya nchi yaliunganishwa, na hii ilikuwa mwanzo wa milki ya Uajemi. Mfalme Koreshi II aliunganisha Uajemi yote chini ya mamlaka yake akavamia sehemu za Uturuki wa leo na Babeli na kuunganisha nchi hizo. Waandamizi wake walipanua milki hadi Misri, Uhindi na Ugiriki.
CHANZO CHA DOLA YA UAJEMI NA UMMED
Kuna dalili za kuwepo Kwa watu katika eneo la Uajemi kuanzia zama za mawe. Akiolojia iligundua vifaa vya Neanderthal na baadaye ya binadamu ya homo sapiens katika eneo hilo la uajemi hasa katika miji ya Esfahan,babol na mashad. Hata hivyo Kijiji cha kwanza ambako watu walilima ilithebitishwa Kwa zamani ya mnamo 7200 BC, Dola la kwanza linalojulikana katika eneo la Uajemi ilikuwa ni “milki ya Elam” katika tambarare ya Khuzestan jirani ya Mesopotamia. Wakazi hao walitumia lugha ya karibu na Sumer kwenye mto Frati.
Mnamo mwaka 3000 BC tawi moja la wahamiaji “Waarya” liliingia kutoka kaskazini na kukalia nyanda za juu za nchi tawi lingine likaingia Uhindi. Hata hivyo neno "Arya" ni asili ya jina "Iran" jinsi watu wa Uajemi wanaita nchi yao.
CHIMBUKO LA WAMED
Hawa wanoitwa Wamedi ni Kati ya makabila walikuwa Wamedi walioanzisha milki ya Umedi na kutawala theluthi ya magharibi ya uajemi ya leo. Walipaswa kukukabili ubwana wa milki ya Ashuru katika Mesoipotamia. Mnamo mwaka 700 BC makabila ya Wamedi yaliunganishwa mara ya kwanza katika shirikisho wakafaulu kujiweka huru kutoka utawala wa Ashuru(Mesopotamia) wakajenga mji mkuu huko Ekbatana. Chini ya mfalme Cyaxares Wamedi waliunga mkono na mfalme Nabopolassar wa Babeli wakashambulia pamoja milki ya Ashuru na kuiharibu vibaya.
Katika UMEDI kulikuwa na nasaba ya “Waakhameni” nasaba hii ilikuwa Kati ya makabila chini ya Wamedi walikuwa Waajemi waliojiita wenyewe Wapars. Mnamo mwaka 700 BC Na kiongozi wa moja kati ya koo za Waajemi alikuwa mfalme wao lakini bado chini ya ubwana wa Umedi. Mnamo Mwaka 553 BC mfalme wa 5 katika nasaba ya Akhameni Koreshi II aliasi dhidi ya babu yake Astyages mfalme wa Umedi akafauli kumpindua. Sasa Koreshi alijiita "mfalme wa Wamedi na Waajemi" akaendelea kufanya vita dhidi ya majirani yake akatwaa milki za Lydia, Babeli, Baktria na Sogdia hivyo kuunda milki kubwa iliyojulikana duniani yote wakati ule. Mwanawe Koreshi Kambisi II alivamia Misri 525 BC na kuongeza nchi hii katika milki ya Waakhameni.
Mfalme Dareio I aliyefuata alizidi kupanusha eneo hadi kujumlisha Asia Magharibi yote, milima ya Kaukazi, Asia ya Kati pamoja na Afghanistan, sehemu kubwa za Pakistani ya leo, Afrika ya Kaskazini pamoja na Misri, Libia, pwani la Sudani, Eritrea, sehemu za Balkani. Aliingia pia Ugiriki kwa shabaha ya kuadhibu Athens iliyowahi kusaidia miji ya Wagiriki iliyoasi katika Asia Ndogo dhidi ya milki ya Uajemi. Lakini kwenye mapigano ya Marathon (MARATHON WAR) mwaka 490 BC Waajemi wakashindwa wakarudi Asia.
Mfalme aliyemfuata Xerxes I alirudi Ugiriki miaka 10 baadaye kwa jeshi kubwa na jahazi za kijeshi. Alijenga daraja la jahazi juu ya mlango bahari wa Bosporus akashinda Wagiriki kwenye mapigano ya Thermopili mnamo 11. Agosti 480 BC ambako askari 300 kutoka Sparta chini ya mfalme Leonidas walifaulu kuwazuia Waajemi Kwa siku kadhaa hadi sehemu kubwa ya Wagiriki waliweza kujiokoa. Waajemi waliendelea na vita hadi Athens iliachwa na wakazi wote lakini kwenye mapigano ya baharini ya Salamis jeshi lote la bahari la Kisajemi lilizamishwa na Wagiriki. Mwaka ulikofuata 479 BC Wagiriki walifaulu kushinda jeshi la Waajemi kwenye mapigano ya Plataia (PLATAIA WAR). Katika miaka iliyofuata Wagiriki walifaulu kuwalazimisha Waajemi kuondoka katika pwani la Ionia penye miji mingi ya Kigiriki.
Chini ya wafalme wa Kiakhameni waliofuata milki kubwa ilipaswa kushindana na majiribio ya sehemu mbalimbali za milki yao zilizojaribu kuasi na kutaka uhuru. Hata hivyo Bonde la mto Indus liliondoka katika milki na kuwa huru bada y kuasi na kushinda vita. Mfalme Xerxes III alifaulu kurudisha Misri katika milki 343 BC na kukandamizi uasi wote.
KUANGUKA NA KUPOLOMOKA KWA DOLA YA UAJEMI NA UMMED NA KUZALIWA KWA IRAN
Dario III alikuwa mfalme wa mwisho wa nasaba hii (330 BC - 336 BC). Mnamo 334 BC Aleksanda Mkuu mfalme wa Makedonia ya Kale (UGILIKI) alishambulia milki ya Uajemi. Katika mapigano ya Issos 333 BC alishinda jeshi la umed chini ya mfalme Dario mara ya kwanza akaendelea kuvamia Misri na kuiteka 332 BC. Na hatimaye 331 BC alielekea tena Mesopotamia alipokutana na Dario na jeshi lake kwenye mapigano ya Gaugamela na kumshinda tarehe 1 Oktoba 331 BC.
Akaendelea na kuingia Babeli bila mapigano alipojitangaza kuwa "mfalme wa Asia" Na ndio ikawa mwanzo wa kuinuka kwa dola la Ugiliki . Katika Januari 330 BC alifika kwenye mji mkuu wa miliki ya uajemi na ummed Persepolis akaendelea kumfuta Dario hadi Baktria. Hapa mfalme wa Uajemi aliuawa na gavana wake na kisha Aleksanda alimuua huyo gavana na kisha akarudi na maiti ya mfalme wa uajemi mkaka mji mkuu wa dola ya uajemi Persepolis alipomzika kwa heshima yote na kujitangaza mtawala mpya wa Uajemi. Hii ilikuwa mwisho wa nasaba ya Akhameni na ndio ikawa mwisho wa anguko la dola hiyo ya Uajemi na umedi.
Milki hiyo ilikwisha baada ya kushindwa na Aleksanda Mkuu mtwa wa dola ya Ugiliki (Greeco) Alexander aliunda jeshi lake na kutangaza azma yake ya kutawala dunia akitokea Ugiriki, kwamba dunia nzima ingefuata amri zake. Viongozi wa dola nyingine wawe kama magavana, wenye kufuata maagizo yake. Kuanza kuinuka kwa Ugiliki ndio ilikuwa mwisho wa dola ya Uajemi. Na ndio ikawa kupolomoka kwa dola hiyo. Hata hivyo katika uajemi Lakini baadae jamii za koo ya nasaba za Waparthia na Wasasanidi waliendelea kufufua milki ya Uajemi tena na tena. Baada ya uvamizi wa Waarabu Ujaemi wakatawaliwa kwa muda kama sehemu ya ukhalifa wa Uislamu. lakini baada ya karne kadhaa kupita nasaba za kieneo zilichukua utawala kwa jina la khalifa ila hali halisi ilikuwa kama watawala wa kujitegemea. Baada ya uvamizi wa Wamongolia katika miaka ya 1300 nasaba ya wana wa Timur iliunganisha Uajemi pamoja na Afghanistan na Asia ya Kati. Tangu mwaka 1600 kitovu cha utawala kilirudi kwa Uajemi wenyewe chini ya nasaba za Safawi na Khadjari.
Baada ya vita kuu ya kwanza ya dunia afisa wa kijeshi Reza Khan alimaliza utawala wa Wakhadjari akaanzisha nasaba ya Pahlavi. Alijaribu kuleta matengenezo ya kimaendeleo nchini akaiga katika mengi kutoka kwa Atatürk katika Uturuki ambayo ilikuwa ni jirani yake. Utawala huo wa kifalme ulikwisha mwaka 1979 wakati wa mapinduzi ya Kiislamu chini ya uongozi wa Ayatollah Khomeini yaliyoanzisha mfumo mpya wa Jamhuri ya Kiislamu.
MAPINDUZI MATAKATIFU YA IRAN YA 1979.
Kimsingi Iran ilikua chini ya ya kifarme kwa miongo mingi (Monacrch) kwa zaidi ya miaka 2000 chini ya Shah Mohamed reza Khan Pahlavi, Ufalme huu ulikua rafiki wa Israel , USA na South Africa ya Makaburu Shah alikua kipenzi cha west na kibaraka mkubwa. Alitumika sana kuzorotesha uhuru wa baadhi ya nchi. Mfano miaka ya 1970 kulikua na azimio la kuiwekea vikwazo Israel vya mafuta. Nchi zote za Opec zilikubaliana kuiwekea Israel vikwazo kutokana na ukaliaji wake wa maeneo ya Masri , Palestine, Syria na Lebanon, Vikwazo vile havikufanikiwa kwani IRAN chini ya Shah akitumiwa na West powers alivivunja na akawa ana supply mafuta Israel. Hivyo mpango ule uka fail.
Pili Wakati UN iliwekea vikwazo South Africa ikiwamo kuuzuwa Mafuta ili kuibana kuachana na siasa zake za kikaburu...jumuiya yote ya Opec na wazalishaji mafuta walikubaliana kuto kuuza mafuta Kwa makaburu. Ni IRAN tena chini ya Shah ikavunja mpango huo na ikawa inauza mafuta kwa makburu. (Kuja kwa Ayatollah na Islamic Republic ilikatisha kuwapatia mafuta Mkaburu na ikawa ndio chachu ya kuanguka) Khomein mwanzo alikua akiishi Iran na kutokana na upinzani wake kwa Shah akafukuzwa hivyo akaamua kuishi Iraq. Huko Iraq chini ya Sadam ambaye alikua darling wa West akalazimishwa kumfukuza na akaamua kuhamia France.
Akiwa huko ndiko aliainzisha harakati kubwa za kumuondoa Shah kwa kutumia mwavuli wa imani ya wairan ya Kishia. Akapata uungwaji mkubwa wa kuungwa mkono na raia wengi ambao walichoka na mambo ya shah. Hata hivyo Ayatollah aliamua kwenda France ikiwa huko france aliamua kuendelea na siasa na hta hivyo france hawakumzuia kufanya siasa akiwa huko, inawezekana France haikufaidika sana na Shah ambaye alielemea sana USA. HIVYO ILIACHIA Ayatollah anedeshe harakati zake nchini ufaransa.
Akaitisha migomo na maandamano makubwa yasio na kikomo...askari wa Marekani na wale wa Shah walifanya kila mbinu za mateso na mauaji lakini raia hawo wa iran awakusimama wala kuvunjika moyo Utawala wa shah ukaanza kuporomoka na Shah akakimbia nchi baada ya hali ya nchi kuchafuka siku Ayatollah alipotangaza anarudi IRan. Kitu interesting ni kuwa France walitoa ndege yao Airbus iliyo msafirisha Khomein kutoka France akiwa na familia yake na timu yake yote ya wapinzania iliokuwa ikiishi uhamishoni. Juhudi za USA, Israel na Iran na UK kuitaka France asimruhusu kurudi hazikusikilizwa na Ufarance ...hatimae Khomein alitua Teheran na Utawala kibaraka wa Shah Ukaanguka.
Hivyo utaona USA na other western countries hawakusaidia Kuanzishwa kwa Taifa la kiislam la Iran. Ufaransa alishiriki kusaidia moraly kwa tamaa ya kuwa na influence kwa utawala mpya. Ingawa hakufikiria kama utawala utakaongia utakua too extreme ...lakini upande mmoja France ndio bado wananufaiaka sana kibiashara na Iran mpya ingawa vikwazo vilizorotesha mahusiano yao. Kipindi kifupi baada ya mapinduzi Uajemi ilishambuliwa na Iraki na vita vya miaka 8 ilisababisha vifo vingi. Uhusiano na nchi za magharibi, na hasa Marekani, umekuwa mgumu tangu mapinduzi, hasa baada ya wanafunzi Waajemi kushambulia ubalozi wa Marekani mjini Teheran na kuwateka Wamarekani kama mateka. Pamoja na hivyo uhasama uliongezeka pale Fatwa ya Ayatollah Khomeini kudai kifo cha mwandishi Salman Rushdie iliongeza sifa za ukali za Uajemi.
Tangu uchaguzi wa Rais Mahmoud Ahmadinejad mwaka 2006 aliyetamka matishio dhidi ya nchi ya Israeli kuna mashaka juu ya mipango ya Uajemi kupanua teknolojia yake ya kinyuklia kwa hofu ya kwamba serikali yake inalenga kujenga bomu ya nyuklia. Mapatano yalichukua miaka hadi kufikiwa mwaka 2015.
MFUMO, UTAWALA NA SIASA MPYA IRAN BAADA YA 1979 (JAMUHURI YA KISLAMU YA IRAN)
Kwa sasa Jamhuri ya Kiislamu ya iran inayoongozwa na katiba yenye sehemu za kidemokrasia na sehemu za kidini. Mamlaka kuu iko mikononi mwa Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi anayesimamia siasa ya nchi kwa jumla yeye ni amiri jeshi mkuu na msimamizi mkuu wa huduma ya usalama pia anaratibu siasa ya nje. Anateua wakuu wa jeshi, redio na televisheni, viongozi wa salat wa msikiti mkuu katika kila mji, jaji mkuu na mwendesha mashataka mkuu halafu nusu ya wajumbe wa Halmashauri ya Walinzi wa Katiba wanaokubali au kukataa sharia zote zilizopitishwa bungeni wakiwa na mamlaka kusimamisha wagombea kwa uchaguzi wa kitaifa. Pia Anaweza kumwachisha rais.
Kiongozi mkuu huyo (Ayatollah) huchaguliwa na Mkutano wa Wataalamu wa Uongozi kwa muda wa maisha yake. Ayatollah Ally Khamenei ni Kiongozi Mkuu wa pili tangu mapinduzi ya Kiislamu. Pia Serikali inayoongozwa na rais wa Uajemi aliye na nafasi ya pili baada ya Kiongozi Mkuu. Huchaguliwa na wananchi wote kwa kipindi cha miaka 4 na anaweza kuchaguliwa upya. Wagombea wanahitaji kukubaliwa na Halmashauri ya Walinzi wa Katiba. Rais anaongoza serikali na kazi yake. Katika mambo ya siasa ya nje, jeshi na siasa ya nyuklia yuko chini ya mamlaka ya kiongozi mkuu.
Bunge inayoitwa "majlis" ina wabunge 290 waliochaguliwa kwa muda wa miaka 4. Wagombea wote wanahitaji kibali cha Halmashauri ya Walinzi wa Katiba. Majlis inatunga sheria za nchi na kukubali makisio ya serikali na mikataba ya kimataifa. Sheria zote zilizopita bungeni zinahitaji tena kibali cha halmashauri ya walinzi. Halmashauri ya Walinzi wa Katiba ni chombo muhimu sana kinachohakikisha mamlaka kuu ya kiongozi mkuu. Ina wajumbe 12 ambao ni wanasheria. 6 wanateuliwa moja kwa moja na Kiongozi Mkuu. 6 wengine wanachaguliwa na bunge kati ya majina wanaopelekwa mbele na jaji mkuu - anayeteuliwa na Kiongozi Mkuu. Kwa hiyo kiongozi mkuu anaamua juu ya wajumbe wote waliomo katika halmashauri hii, hakuna anayeweza kuwa mjumbe bila kibali chake ama moja kwa moja au kupitia jaji mkuu aliyeteuliwa naye.

No photo description available.

No comments:

Post a Comment