Breaking

Tuesday, January 28, 2020

Mfahamu Zaidi Kobe Bryant: Bingwa mara tano NBA

 


 


Kobe Bryant almaarufu kwa jina la black mamba ni mchezaji mstaafu wa mpira wa kikapu ambae ameweza kupata mafanikio makubwa. Mafanikio hayo yamepelekea hata watu kuanza kumfananisha mchezaji huyu na Michael Jordan. Katika maisha ya Kobe Bryant ya uchezaji wa kulipwa wa kikapu, Kobe  ameweza kushinda ubingwa wa ligi ya kikapu ya Amerika mara tano akiwa na timu yake ya Los Angeles Lakers na kujiweka kuwa mojawapo wa wafungaji bora katika historia ya ligi hiyo.


 


Kobe Bryant alizaliwa mnamo tarehe 23 Agosti mwaka 1978, Philadelphia, Pennysylvania. Katika maisha yake ya utoto, Kobe Bryant alikulia Italia ambako baba yake alikuwa akicheza mpira wa kikapu. Mnamo mwaka 1991, Kobe Bryant alirudi Marekani na kupata jina haraka kama mchezaji bora wa shule za sekondari nchini humo. Alipomaliza sekondari, Kobe Bryant alichaguliwa moja kwa moja kama mtu wa kumi na tatu kujiunga na ligi ya kulipwa nchini humo. Wakati Kobe anaanza mpira wa kikapu, watu walijiuliza inawezekanaje kijana mwenye umri mdogo wa miaka kumi na saba kufanya mambo kama anayofanya. Watu walishangazwa sana na kiwango cha juu cha kijana huyu.


 


Kobe Bryant aliungana na Shaquile O’neal na Kocha Phil Jackson katika timu ya L.A Lakers na kuweza kuchukua ubingwa wa ligi ya nba mara tatu mfululizo kuanzia mwaka 2000 mpaka 2003. Mchanganyiko wa Kobe na Shaq ulikuwa maarufu sana na watu waliupenda na kuufurahia sana. Kocha Phil Jackson alikuwa anamuita Kobe Bryant “Mr Outside” na Shaquille O’neal  “Mr Inside”.


 


Mwaka 2003 Kobe Bryant alipata kesi ya ubakaji. Hii kesi iliharibu uhusiano wa kibiashara baina ya  Kobe na makampuni mengi . Kobe aliwashangaza watu pale alipotoka mahakamani kutoa ushahidi na siku hiyo hiyo kuingia uwanjani na kutupia pointi 32 kwenye mchezo. Kipindi hiki kilikuwa kigumu sana kwa Kobe kwani hata mashabiki wa L.A Lakers walikuwa wakimzomea uwanjani na kutaja jina la huyo msichana aliesema kabakwa. Kipindi hiko hiko maelewano baina ya Kobe na Shaquille O’neal yakaharibika mpaka kupelekea Shaq kuuzwa kwenda timu nyingine Miami Heat mwaka 2004. Baada ya ushahidi kukosekana kesi ya ubakaji ya Kobe Bryant ilifutwa lakini madhara yalikuwa yameshafanyika.


 


Baada ya vyote hivyo kutokea, Kobe Bryant aliendelea kushinda mataji mawili ya ubingwa wa nba mnamo mwaka 2008 na 2009 akiwa na timu yake ya L.A Lakers. Ingawa Kobe Bryant akaanza kukumbwa na matatizo ya mara kwa mara ya enka, alifanikiwa kumpita Michael Jordan na akawa mtu wa tatu kuongoza katika ufungaji kwenye historia ya ligi ya nba mnamo December mwaka 2014. Mwaka 2016 Kobe Bryant alitangaza kustaafu kucheza mpira wa kikapu na  mnamo tarehe 13 April 2016 alicheza mchezo wake wa mwisho ambapo alifunga pointi 60.


 


No comments:

Post a Comment