Breaking

Tuesday, January 28, 2020

Mwanamke ukifaulu hili, ndoa yako itadumu

Moja kati ya vitu vinavyowavutia wanaume kwa wake zao ni mapishi. Mke ukiweza kumteka mumeo katika suala la mapishi, mumeo hatokuwa na sababu ya kutokula chakula unachokipika, lakini pia atakauwa mwenye kujitahidi kurudi nyumbani mapema kuja kula chakula kitamu kilichopikwa na mkewe.

Mke unapokuwa upo jikoni unaandaa chakula, ni lazima ujue kuwa atakaekula chakula hicho ni mumeo, hivyo ni vizuri ukatumia ujuzi wako wote kuhakikisha mumeo anakula chakula kizuri.

Wanawake wengi wanakawaida ya kupika chakula kizuri siku za sikukuu, hapo ndio anajitahidi kutumia uelewa wake wote katika kupika ili tu aonekane na majirani na si mumewe, au siku akisikia mume anakuja na mgeni au rafki yake ndio unataka upike vizuri, hilo si jambo jema.

Jitahidi kumpikia mumeo kila siku chakula kizuri, mvutie mumeo kwa chakula chako, mfanye kila anapopata muda wa mapumziko kazini arudi nyumbani kula. Utundu wa mwanamke unaanzia jikoni.

No comments:

Post a Comment