Breaking

Wednesday, January 29, 2020

SIMULIZI: NIMEKOSA NINI?: sehemu 4.


ILIPOISHIA TOLEO LILILOPITA.....
‘Kumbe hakuna hata mmoja mwenye moyo wa huruma hapa, wote wamepinda na wanaroho za kikatili.’ Nlijiwazia baada ya kumuona hata yule aliyekuwa kimwa muda wote anashabikia kunyimwa fursa ya kumpa taarifa mke wangu.
SASA ENDELEA NAYO.....
Safari iliendelea kuelekea kituo cha kati (central) huku ukimya ukiwa umetawala. Hatimaye tulifika kituoni, nikashushwa na kupelekwa ndani moja kwa moja kwenye chumba cha mateso. Nilikuwa sijawahi kuingia katika chumba kile ila nilikuwa nasimuliwa tu na watu kwamba ukipelekwa mle mateso yake ni balaa, yaani utajuta kuzaliwa. Juu ya mlango wa chumba hicho palikuwa pameandikwa “GEREJI YA WAHARIFU”
Tulipofika kwenye chumba hicho tulipokelewa na njemba nne ambazo zilikuwa zimeshiba kweli kweli. Kati ya njemba hizo mmoja alikuwa ni mwanadada. Vifua vyao vilikuwa vimetuna kwelikweli mithili ya Hawafu mwenye nguvu tuliyekuwa tukimsoma katika kitabu cha shule ya msingi. Fadhaa ikaanza kuniingia moyoni, nikawa nakiona kikombe kikali cha mateso kilichopkuwa mbele yangu, lakini hata kosa nilikuwa silijui kiundani zaidi.
Waliponifikisha kwenye chumba hicho walinikabidhi kwa mabausa hao kisha wao wakatoka. Hapo tena nikawa nipo mikononi mwa watu wengine ambao sura zao zilikuwa zinatisha zaidi hata ya wale wa awali.
“Sisi ni watu wema sana endapo utakuwa mkweli kwetu, lakini ukijifanya jorowe tutakushikisha adabu mpaka ujute kuzaliwa. Ni heri ukasema ukweli wote mapema iwezekanavyo kabla hatujaanza kufanya kazi yetu, huo ndiyo usalama wako.” Aliongea mwanadada aliyekuwa ni miongoni mwa njemba hizo ambaye alikuwa na uso uliokomaa.
Muda wote huo akili yangu ilikuwa na kazi ngumu ya kujiuliza ni ukweli upi nitakaowaambia watu hao. Nilijua fika kuwa hata kama nitawaeleza ukweli wenyewe hawatausadiki kwa kuwa nilikuwa sijahusika kabisa na uvamizi wa ofisi yetu. Wakati mwingine nilianza kujiuliza labda kuna jambo jingine tofauti na hilo la ujambazi katika kampuni yetu. Niliamua kusubiri ili nisikie wanachoniuliza.
Wakati huo nilikuwa nimekalishwa kwenye kiti cha chuma kilichokuwepo katikati ya chumba hicho huku nyuma yake kukiwa na nguzo ya chuma yenye urefu kimo cha mtu mzima. Niliweza kukadiria urefu wake ulikuwa wapata futi tano ama sita kasoro ushei.
Mikono yangu ilikuwa bado imefungwa pingu. Mara niliwaona jamaa wawili wakichukua minyororo midogo midogo iliyokuwa imening’inizwa ukutani. Walikuja moja kwa moja na kuanza kunifunga miguuni. Walipomaliza miguuni walizifungua pingu nilizokuwa nimefungwa mikononi kisha mwanamke aliyekuwemo akaja na kunivua koti pamoja na tai yangu nikabaki na shati tu.
“Ngoja nimvue koti mume wangu maana joto litamsumbua.” Alitamka mwanamke huyo wakati analifanya hilo zoezi.
Alipomaliza kunivua koti vijana waliokuwa na minyororo waliirudisha mikono yangu nyuma na kuifunga kwenye nguzo ya chuma iliyokuwa nyuma yangu.
Mpaka hapo moyo wangu ulikuwa ukitabiri sulubu nzito. Vile vibao viwili tu vilikuwa vimenichachafya sembuse mateso ya kwenye gereji ya wahalifu! Nafsi yangu ilizidi kusononeka nipoyawaza hayo.
Baada ya hapo wale jamaa watatu walitoka na kumuacha mwanadada peke yake. Mwanadada huyo alivua blauzi na kubaki na sidiria tu. Kitendo hicho kilizidi kunishangaza.
Kwa mwendo wa tararibu alikuja mpaka nilipokuwa nimekalishwa, akanikumbatia na kunipiga busu lililousisimua mwili wangu wote. Woga na hofu ya mateso vyote viliniishia.
Kama ilivyo ada kwa mwanaume aliyekamilika kila idara, shetani wa mahaba alianza kunisumbua, nikajikuta wazee wanaanza kushangilia wakitaka uhuru wa kutoka kifungoni.
Mwanadada huyo hakuishia kunichumu tu, alinikumbati na kufanya ‘manyanga’ ya kwenye kifua chake yaliyokuwa yamebanwa na sidria yagusane na kifua changu, hali ambayo ilileta msisimko fulani katika mwili wangu na kusababisha mahanjamu zizidi kupanda. Ashki ya mapenzi ikawa imenikamata mtoto wa kiume si mchezo.
Mara alikaa kwenye mapaja yangu na kuanza kuvifungua vifungo vya shati langu. Alipofikisha kwenye tumbo aliacha na kuipeleka mkono wake kwenye kifua changu kisha akaanza kuchezea chezea bustani ya mahaba ambayo ilikuwa ni mali ya mama Chris.
“Huyu mwanamke mbona anazidi kunitega? Anajua sitafanya chochote kwa sababu wamenifunga minyororo! Anabahati yake, isingekuwa hii minyororo tungemaliza biashara humuhumu.” Nilizidi kujiwazia huku burudani murua ya mikono ya mwanamke huyo ikiusisimua mwili wangu kwa kupapasapapasa kifua changu sanjari na tumbo.
Mara alisitisha zoezi hilo na kuendelea na kufungua vifungo vya shati langu. Hatimaye alivimaliza vyote na kunibakisha nikiwa kifua wazi.
“Vipi unajisikia raha eeh! Unatamani zoezi liendelee! Usijali mpenzi wangu nipo kwa ajali yako!” Aliongea mwanadada huyo kwa sauti ya kimahaba na kuzidi kunimaliza. Nahivi ilikuwa ni siku ya nne sijakafanya kale kamchezo na mke wangu kutokana na kuwa mikoani katika hayo masuala, basi mwanamke huyo alizidi kunipa hamasa; si unajua tena mwanaume rijali akihamasihwa kidogo tu huhamasika zaidi! Yaani wee acha tu!
Huku akiwa kakaa kwenye mapaja yangu na nyanga lake moja la kifuani likiwa limegusa barabara kwenye kifua changu nilichokuwa nimekitanua ipasavyo baada ya kufungwa mikono yangu kwenye nguzo; mwanadada huyo alianza kuniuliza!
“Una mke?”
“Ndiyo ninaye!” Nilimjibu huku nikipumua pumzi fupifupi kutokana na kuzidiwa kimahaba.
“Sasa mimi nataka nikusaidie ili ukaendelee kula raha za dunia na mkeo, lakini hata utanihitaji na mimi niwe hawara yako tuwe tunamuibia mkeo mara mojamoja nipo tayari; ninachotaka kutoka kwako uniambia ukweli wote juu ya hili!” Alisita kidogo kisha akabadili pozi, sasa akawa amepiga magoti chini na kukilaza kifua chake chote kwenye kifua changu kisha akaniangalia kiaina.
Baada ya hapo aliendelea kwa kusema,
“ upo tayari kurudisha vitu vyote mlivyoiba usiku wa leo kwenye kampuni yenu?”
Jibu la swali hilo lilikuwa ni jepesi sana lakini lilinipa kigugumizi kulitamka. Nikajikuta nikiganda kimya kwa sekunde kadhaa. Mwanamke huyo akaongea tena kwa sauti ya kubembeleza,
“Unajua bosi wako anakupenda sana, sasa maagizo aliyotupa sisi ni kwamba hahitaji mambo yafike mbali, anachotaka yeye vitu vyote vyote vilivyoporwa pale kwenye kampuni virejeshwe, ukishafanya hivyo utarudishwa kazini na kuendelea na kazi kama kawaida.”
Kwa kweli nilikuwa katika wakati mgumu sana. Hata kama ungekuwa ni wewe mpendwa msomaji lazima ungeumiza kichwa. Watu wanakutuhumu kuwa umefanya tukio wakati huna ujualo.
Hisia za mapenzi zilianza kunishuka licha ya kulaliwa kifuani na mwanamke huyo. Akili yangu sasa ilihamia kwenye kutafuta jibu la kumjibu mwanamke huyo ambalo lingeweza kumridhisha. Kama ningesema nimwambie sijaiba lazima kipigo angeanza kunishushia. Vilevile ningekubali kuwa nimehusika katika kuiba wangetaka vitu virejeshwe, sasa ningevitoa wapi wakati nilikuwa sijashiriki katika wizi huo? Nilizidi kuchanganyikiwa.
ITAENDELEA......

No comments:

Post a Comment