Breaking

Wednesday, January 15, 2020

SOMA MAAJABU YA HAWA MARAIS WA MAREKANI, JE NI HISTORIA AU YALIPANGWA?

Image result for historia ya abraham lincoln

Abraham Lincoln alichaguliwa kuingia katika bunge la Marekani mwaka 1846. John Kennedy alichaguliwa kuingia katika Bunge hilo mwaka 1946. Hiyo ni tofauti kati ya miaka 100.
Mwaka 1856 Lincoln hakupata kura za kutosha kupendekezwa kugombea Urais. Mwaka 1956 Kennedy naye alishindwa kuteuliwa kugombea Umakamu wa Rais.
Abraham Lincoln alichaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwaka 1860. Jonh Kennedy akachaguliwa kuwa Rais mwaka 1960.
Katika mbio za Uchaguzi Lincoln alimshinda Stephen Douglas aliyezaliwa Mwaka 1813. Kennedy naye alimshinda Richard Nixon aliyezaliwa 1913.
Wote wawili Lincoln na Kennedy walijishughulisha na Haki za Kiraia na wote walisoma Sheria.
Wake zao Marry Todd Lincoln na Jacqueline Bouvier Kennedy walifiwa na watoto wakati waume zao wakiwa Ikulu.
Mtoto wa Lincoln aliitwa Edward Baker Lincoln. Mtoto wa Kennedy aliitwa Patrick Bovier Kennedy. Watoto wao wote walikuwa wakitumia majina ya koo za mama zao Bouvier(Kennedy) na Baker(Lincoln).
Wote wawili, Abraham Lincoln na John Kennedy waliuawa kwa kupigwa Risasi siku ya ijumaa na walipigwa Kichwani.
Katibu wa Abraham Lincoln aliitwa Kennedy, na Katibu w John Kennedy aliitwa Lincoln. Marais wote wawili waliuawa na watu wanaotoka kusini mwa Marekani na wote baada ya Kuuawa, warilithiwa na watu waliotoka waliotoka kusini mwa Marekani.
Marais wote wawili walikuwa na Makamu wa Rais waliokuwa na majina ya Johnson. Makamu wa Rais wa Lincoln aliitwa Andrew Johnson ambaye alikuwa mjumbe wa Baraza la wawakilishi mwaka 1847. Makamu wa Rais wa Kennedy aliitwa Lyndon Johnson ambaye alikuwa mjumbe wa Baraza la Wawakilishi mwaka 1947.
Warithi wao wote (Makamu wao wa Rais) Waliitwa Johson. Andrew Johnson ambaye alimrithi Lincoln alizaliwa mwaka 1808. Lyndon Johson aliyemrithi Kennedy alizaliwa 1908.
Joh Wilkes Booth, ambaye ndiye muuaji wa Lincoln, alizaliwa mwaka 1839. Lee Harvey Osward, ambaye alimuua Kennedy alizaliwa 1939.
Lincoln alipigwa risasi akiwa katika ukumbi ulioitwa Ford kwa heshima ya aliyekuwa mtengenezaji magari maarufu aliyeitwa Henry Ford. Kennedy alipigwa akiwa katika gari lililoitwa "Lincoln" lililotengenezwa na kampuni ya Ford iliyomilikiwa na Henry Ford.
Muuaji Booth, baada ya kumuua Lincoln, alikimbia kutoka Ukumbini alimofanya mauaji na akakamatwa katika bohari. Muuaji Osward aliyemuua Kennedy alikimbia kutoka bohari na kukamatwa ukumbini. Wauwaji wote wawili Booth na Osward waliuawa kabla ya kesi zao hazijaanza kusikilizwa.
Rais Lincoln alizaliwa Februari 12, 1809 na kufariki April 15, 1865 akiwa na miaka 56, Rais Kennedy alizaliwa Mei 29, 1917 na kufariki November 22, 1963 akiwa na miaka 46.
Mwezi mmoja kabla ya Lincoln hajauawa alikuwa eneo lililojulikana kama Monroe lililoko Maryland. Kennedy mwezi mmoja kabla hajauawa alionekana akiwa na mcheza sinema maarufu aliyeitwa Marylyn Monroe. Sinema peke yake iliyokamilika ambayo inaonyesha mauaji ya John Kennedy ilitengenezwa na mtu aliyeitwa Abraham Zapruder, na maelezo yaliyokamilika yanayoelezea mauaji ya Abraham Lincoln yaliandikwa na John Zelfindorter.
Mtoto wa Lincoln aliyeitwa Tad alizikwa Julai 16, 1871, mtoto wa Kennedy, JFK Jr alifariki julai 16, 1999.
John Kennedy na Abraham Lincoln wote walisoma Sheria na wote waliwahi kufanya kazi Jeshini.
Kennedy alichaguliwa kuwa Rais November 8, Lincoln alichaguliwa kuwa Rais November 8. Kennedy alikuwa mtoto wa pili katika familia yake na Lincoln naye alikuwa mtoto wa pili katika Familia yake.
Wote wawili walitumia Majina ya babu zao. Kennedy alikuwa na watoto walioitwa Robert na Edward, kadhalika Lincoln alikuwa na watoto walioitwa Robert na Edward. Kennedy alizaa watoto wanne na Lincoln alizaa watoto wanne.
Lincoln alikuwa na Daktari wake aliyeitwa Charles Taft, Kennedy naye alikuwa na Daktari wake aliyeitwa Charles Taft.
Lincoln alikuwa na rafiki yake na mshauri aliyeitwa Willium Graham. John Kennedy alikuwa na rafiki yake na mshauri aliyeitwa Bill Graham.
Chanzo kimoja cha habari kinasema mwaka mmoja kabla Lincoln hajauawa alipokea barua 80 zilizotishia uhai wake na chanzo hicho hicho kinasema mwaka mmoja kabla Kennedy hajauawa alipokea barua 800 za kutishia uhai wake. Barua za Kennedy ni mara kumi ya zile za Lincoln lakini namba yake ni 8.
Lincoln aliuawa mbele ya mkewe na Kennedy aliuwa mbele ya mkewe.
JE HAYO YALITOKEA BAHATI MBAYA AU YALIPANGWA AU HISTORIA ILIJIRUDIA?

No comments:

Post a Comment