Breaking

Sunday, January 12, 2020

Wanawanake watano hatari zaidi duniani: Walikuwa majasusi, waigizaji filamu na wanaharakati wa kijamii


Killing EveHaki miliki ya pichaGODSTAR / SID GENTLE FILMS / JASON BELL IMAGE
Image captionFilamu ya mauji ya Eve

Makala mpya ya BBC inayofahamika kama "Killing Eve'' ambayo inasimulia mateso wanayopitia wahusika kama vile Villanelle anayejulikana kama Jodie Comer,
Baadhi ya watazamaji wanauliza ni vipi wanawake wanaweza kuwa hatari jinsi hiyo.
Hayo ni yale yaliyoigizwa katika filamu lakini je, kuna wanawake hatari kama hao duniani?

mcheza densi Margaretha Geertruida MacLeod aliyejita "Mata Hari"Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Mata Hari (1876-1917)

Alikuwa mchezaji densi za kiajabu aliyekiuka maadili ya jamii yake kwa kuigiza filamu za Marekani zinazofahamika kama Hollywood.
Alipata umaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake kusakata densi, iliyompatia nafasi ya kushiriki katika filamu maarufu ya Mata Mari mwaka 1931 .
Jina lake halisi ni Greta Garbo, mzaliwa wa Holland.
Alifahamika kama Margaretha Geertruida MacLeod katika filamu ya Mata Hari.
Margaretha alikuwa mke wa kapteni wa jeshi aliyekuwa akimnyanyasa sana.
Siku moja alimpiga hadi akapoteza ujauzito wa mtoto wake, ukatili uliyomfanya kubadilisha mtazamo wake kuhusu wanaume.
Sawa na "Mata Hari, alikuwa mchezaji densi katika miji ya Milan na Paris, na alitumia kazi yake kukwepa sheria ya ustaarabu kwa kutambulisha maonyesho ya densi yake kama ''densi takatifu''
Alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume mashuhuri.
Mmoja wa wapenzi wake alimpeleka Ujerumani kumpatia fedha na taarifa kuhusu washirika wake.
Wakati huo wa vita vya kwanza vya dunia vilikuwa vinaendelea. Inadaiwa kuwa alipewa jukumu la kuchunguza mienendo ya vikosi vilivyokuwa vikikabiliana na Ujerumani, hatua iliyomfanya kupata kazi ya ujasusi wakati wa vita vya kwanza vya Dunia.

Mata Hari nembo ya udanganyifu wa wanawake na sliti wa kisiasaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMata Hari nembo ya udanganyifu wa wanawake na sliti wa kisiasa

Japo hakumua mtu yeyote lakini inasemekana kazi yake ya ujasusi ilichangia kuawa kwa wanajeshi 50,000.
Ufaransa ilimshuku kwa kuhusika na mauaji hayo na baadaye alikamatwa mjini Paris Februari 1917.
Aliuawa na kikosi cha 'firing squad' mwezi Oktoba mwaka huo huo.
Tangu kuuawa kwake zaidi ya miaka mia moja iliyopita, kumekua na mjadala iwapo alikuwa na hatia au la.
Lakini ukweli ni kwamba amekuwa sura ya wanawake wanaotumia mapenzi kusaliti jamii kisiasa .

Charlotte Corday (1768-1793)

Jina lake halisi lilikuwa Marie-Anne Charlotte de Mademoiselle Corday .
Kitu cha kushangaza kumhusu mwanamke huyu ni kwamba alihusika moja kwa moja na mapinduzi ya Ufaransa.
Lakini alikuwa na tabia ya kumleta karibu mwanamume aliyetaka kumuangamiza.

Charlotte Corday akiwa gerezani, baada ya kukamatwaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionCharlotte Corday akiwa gerezani, baada ya kukamatwa

Muathiriwa wake, Jean-Paul Marat , alikuwa kiungo mashuhuri katika kundi pinzani la Jacobin.
Jacobins walikuwa wafuasi wa sera ya magauzi ya siasa kali ambayo baadaye yaligeuka na kutibua mapigano makali yaliyosababisha mauaji ya watu 16,500.
Corday alishtakiwa kwa mauaji ya Marat japo wakati wa kujitetea alisema kuwa "nimemuua ili kuyaokoa maisha ya maelfu ya watu".
Hata hivyo alihukumiwa kunyongwa, kwa kosa la mauaji. Alifariki akiwa na umri wa miaka 24.

Shi Jianqiao (1906-1979)

Alifahamika kama Shi Gulan, lakini wandani wake walimbatiza jina la Shi Jianqiao kumaanisha 'Upanga' unaoashiria ahadi yake ya kulipiza kisasi kifo cha babake
aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na kiongozi Sun Chuanfang, mwaka 1925.

Shi Jianqiao alitumia miaka 10 kulipiza kisasi kifo cha babake.Haki miliki ya pichaPUBLIC DOMAIN
Image captionShi Jianqiao alitumia miaka 10 kulipiza kisasi kifo cha babake.

Miaka kumi baada ya Sun Chuanfang kustaafu, Shi Jianqiao, alimvizia na kumuua kwa kumpiga risasi kichwani akiwa anaomba katika hekalu la kibudha .
Badala ya kutoroka eneo la tukio, Shi Jianqiao, aliamua kuwasmulia wapita njia kuhusu kitendo chake.
Inadaiwa hatua hiyo ilikuwa njama ya kuvutia vyombo vya habari na kutafuta huruma ya watu.
Alifikishwa mahakamani na kusamehewa mashtaka mwaka 1936 , kwa sababu kosa lake lilionekana kama kitendo cha kuwaheshimu ya wazazi wake.
Shi Jianqiao alifariki mwaka 1979.
Brigitte Mohnhaupt (Alizaliwa 1949)
Alifahamika kama mwanamke katili zaidi nchini Ujerumani. Alikuwa mwanachama wa kitengo mashuhuri cha jeshi la Red Army
Brigitte Mohnhaupt alihusishwa na mtandao wa ugaidi uliyofahamika kama 'Autumn German' mwaka 1977.
Wanamgambo wa kundi hilo walisumbua utawala wa Ujerumani kwa kutekeleza visa vya utekaji nyara,mauji na mashambulizi ya mara kwa mara ya miaka ya 1970.

Mohnhaupt hakuwahi kujutia makosa yake.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMohnhaupt hakuwahi kujutia makosa yake.

Mohnhaupt alikamatwa mwaka 1982, na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani pamoja na kifungo kingine cha miaka 15 kwa kuhusika
moja kwa moja na mauaji ya watu tisa ikiwemo moja ambapo alionekana akimpatia mhasiriwa shada la maua kabla ya kumpiga risasi na kumuua.
Licha ya kutojutia makosa yake Mohnhaupt, aliachiliwa huru mwaka 2007 katika hatua iliyozua mjadala mkali kote nchini Ujerumani.
Mohnhaupt yuko hai mpaka leo.
Ajenti Penelope (miaka haijulikani)
Alikuwa ajenti wa wa wapelelezi wa Israel, Mossad aliyefahamika kwa jina la "Penelope". Alihusishwa na jaribio la mauaji dhidi Ali Hassan Salameh, kiongozi wa kundi la Black Septemba
nchini Palestina ambalo liliwateka nyara na kuwaua wanariadha 11 wa Israel wakati wa michezo ya olimpiki ya Munich mwaka1972.
Katika hatua ya kujibu mauaji hayo, Waziri Mkuu wa Israel, wakati huo, Golda Meir aliidhinisha "Operesheni ya Ira de Dios" ambapo mawakala wa Mossad waliwatesa
wanachama wa Black Septemba waliohusika na mauaji ya wanariadha hao.

wachezaji 11 wa Israel waliuawa waka 1972Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES

Kufuatia majaribio matano ya mauaji dhidi yake yaliyotibuka ,Salameh hatimaye alifariki akiwa pamoja na walinzi wake wanne na wapita njia wawili baada ya bomu lililotegwa ndani ya gari kulipuka nje ya nyumba yake mjini Beirut mwaka 1979.
Inadaiwa ajenti Penelope ndiye aliyelipua bomu hilo.

No comments:

Post a Comment