Breaking

Friday, January 31, 2020

Waziri Kigwangala ampa ubalozi Bongozozo

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Hamisi Kigwangalla, amemtangaza mwanamitandao na mhamasishaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Bongozozo, kuwa balozi wa hiari.

Dkt Kigwangalla ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, ambapo amepost video fupi ya Bongozozo na kuandika kuwa.

"Balozi Bongozozo, umefika wakati sasa nitambue rasmi fujo isiyoumiza kama harakati serious ya kuitangaza Tanzania na Kiswahili chetu, kwanza kwa kumtangaza Bongozozo kama balozi wa hiari wa utalii wa Tanzania" ameandika Hamisi Kigwangalla.

"Hivyo naelekeza Bodi ya Utalii Tanzania imuandikie rasmi barua ya kutambua mchango wake na kumtangaza kuwa balozi wa hiari wa utalii, pili kumuandalia safari ya kuja kutalii Tanzania, #TanzaniaUnforgettable" ameongeza.

Bongozozo ni Muingereza ambaye amejipatia umaarufu katika mitandao ya kijamii kwa kuongea kiswahili fasaha, anaishabikia timu ya Taifa ya Tanzania pia ameoa mke kutoka Tanzania ila anaishi naye nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment