Breaking

Friday, January 24, 2020

Zijue ishara za mwanamke anaekupenda ila anashindwa kukwambia

Si rahisi kwa wanamke kukwambia kama anakupenda Bali atakuonyesha ishara kama.....
Nimekuletea ishara chache ambazo waweza kujua kama na wewe unapendwa.

Ni muhimu sana kwako mwanaume kujua kwa uhakika kuwa mwanamke anakupeda kweli kweli,utajuaje kuwa mwanamke anakupenda? Zifuatazo ni ishara ambazo wewe kama mwanaume unapaswa uwe makini ili uweze kuziona na haraka kumtolea uvivu huyo mwanamke.* Mwanamke anayekupenda atahangaika juu yako, atahangaika juu ya usalama wako,raha yako,heshima yako na maendeleo yako.Hii ni moja kati ya ishara kubwa kuwa mwanamke huyo anaupendo na wewe.* Mwanamke anayekupenda atakuonea wivu mara kadhaa,Wivu ni ishara kuwa anakupendawewe na anataka akulinde usiibiwe au asije akakupoteza,anaogopa usije ukatoka katika maisha yake,au kwa maneno mengine usije ukamtoa moyoni mwako na nafasi yake ikachukuliwa.Japo wivu ukizidi sana pia inaweza kuleta tatizo.* Mwanamke anayekupenda atakapokuwa mbele ya marafiki zake au watu wengine atacheka nao lakini atakugeuzia ww macho/uso wake haraka sana. Kufanya hivi ni kuonyesha kuwa anakuhesabia ww kuwa utaweza kumletea furaha katika maisha yake,zaidi ya hilo ni kwamba anatumaini kuwa utamuona kuwa yeye ni mtu aliye rahisi kufurahishwa kwa kuwa yeye ni mtu wa furaha.* Mwanamke anayekupenda ataendelea kukuangalia usoni kwa muda mrefu kuliko ilivyo kawaida ya wanawake wengine,mara nyingi atakuangalia na kutabasamu vizuri. Hii huenda ni ishara moja muhimu sana ya kukuambia kuwa “NJOO NIKO KWAAJILI YAKO.”Hivyo kama ulikuwa unahisi unamhitaji basi ni wakati mwafaka wa kumfuata na kumweleza ukweli na kirahisi nakuhakikishia unabeba mzigo kwani ni mtu tayari aliyekuwa anahisia kali za mahaba juu yako

No comments:

Post a Comment