Breaking

Friday, February 14, 2020

Abiria wa Meli iliyozuiwa Kutia Nanga Waanza Kuteremka Cambodia

Abiria waliokuwamo katika meli ya anasa iliyozuiwa kwa muda wa wiki mbili kutia nanga kwenye mataifa matano kutokana na wasiwasi wa virusi vya Corona wameruhusiwa leo kuanza kuteremka nchini Cambodia.

Meli hiyo ´´MS Westerdam´´ iliyowabeba abiria 1,455 na wafanyakazi 802 imetia nanga kwenye mjini wa bandari wa Cambodia wa Sihanoukville jana Alhamisi.

Kabla ya kuruhusiwa kuingia bandarini maafisa wa Cambodia walitumwa ndani ya chombo hicho kuchukua vipimo vya abiria waliokuwa na dalili za mafua au afya dhaifu ya mwili.

Wizara ya afya ya Cambodia imesema baada ya vipimo hakuna mtu aliyebainika kuambukizwa virusi vya Corona na abiria wameruhusiwa kuanza kutemremka kutoka melini leo asubuhi.

No comments:

Post a Comment