Breaking

Thursday, February 20, 2020

Abiria wawili kwenye meli ya kifahari ya Diamond Princess wafariki kwa virusi vya corona


Abiria wawili ambao walikuwa kwenye Meli ya kifahari ya Diamond Princess ambayo iliwekwa chini ya uangalizi maalum kwa siku 14 nchini Japan wamefariki Dunia kwa Corona, hii inafanya idadi ya waliofariki Japan kufikia watatu.

Abiria walizuiwa kutoka kwenye Meli hiyo kufuatia baadhi yao kubainika kuwa na corona lakini baadae walianza kuambukizana ndani ya Meli ambapo zaidi ya abiria 400 wameathirika na corona.

Kwa sasa wameruhusiwa kushuka, Marekani ilituma ndege mbili kuchukua Raia wake na leo Alhamisi Wachina 114 ambao walikuwa kwenye Meli hiyo wamesafirishwa kwa ndege hadi Hongkong.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment