Breaking

Saturday, February 22, 2020

Aina Kubwa Tatu Za Watu Na Nafasi Zao Katika Mafanikio..!!!!


Wewe ni Mtu wa aina gani?

Hili ni swali ambalo kimsingi kila mmoja lazima ajihoji kwa wakati wake.

Ukisoma katika vitabu mbalimbali vya dini vinasema ya kwamba binadamu wote ni sawa, hii ikiwa na maana ya kwamba ukiangalia katika mfano wa vitu kijinsia, organi pamoja homoni.

Lakini ukija katika ulimwengu wa mafanikio binadamu hatufanani hata chembe na hii ndiyo maana kuna watu maskini na wengine ni matajiri, na nilichokigundua ni kwamba utofati wetu huanza rasmi katika fikra.

Fikra ndiyo inayotufanya tuweze kuwa tofauti.  Hivyo ili binadamu  tuweze kuwa sawa ni vyema kila mtu aweze kutafakari yeye ni mtu wa aina gani? Ukishapata majibu ndipo utapojua  wewe ni wa aina gani na unawezaje kusonga mbele kimasha.

Ili mkupata majibu ya swali hilo, siku ya leo nimekuletea makala ambayo itakusaidia kuweza kujua wewe ni mtu wa aina gani. Hivyo yafutayo ni makundi ya watu ambao wapo hapa duniani katika kuyasaka mafanikio.

Watazamaji.

Aina ya kwanza ya watu wanaopatikana katika duniani hii ni watazamaji. Tabia za watu hawa huwa kama ifuatavyo;

Wao ni waoga katika kujaribu kufanya kitu kipya.

Wao huamini zaidi katika kushindwa kuliko kufanikiwa.

Wao ni wazungumzaji wazuri kwa yale ambayo yanatokea katika jamii.  Watu hawa huzungumza zaidi masuala ambayo huwa hayawasaidii mfano wa mambo hayo ni mpira, siasa na matukio mbalimbali yanayoendelea katika mitandao ya kijamii na mambo ya nje ya mitandao ya kijamii.

Lakini kubwa kabisa watu hawa  huwa hawana ubunifu wowote, na huwa wanaishi katika misingi ya kuwaangalia watu wanaopenda (role model), kwa misingi hiyo utagundua ya kwamba aina hii ya watu huishi maishi ya ganda la ndizi, kwa sababu husubiri mtu afanye jambo fulani ili na wao waanze kufanya.

Wapotezaji.

Kundi hili lina watu lukuki sana. Na watu ambao wapo katika kundi hili huwa wana tabia zifuatazo;
Kazi yao kubwa huwa ni kuwangalia watu wengine wanafanya nini katika maisha yao. Hata hivyo katika kundi hili, watu wengi huwa wapo kwa ajili ya kuwakosa wengine kwa yale wayafanyao, na katika kukosoa huko huwa ni katika kukatisha tamaa zaidi kuliko kujenga.

Watu ambao wapo katika kundi hili ni wale ambao wameathiriwa kwa kiwango kikubwa ugonjwa wa wa kuahirisha mambo ya msingi.

Washindi.

Kundi la tatu la mwisho ni kundi la washindi, kundi hili ndilo lenye watu wachache na wenye mafanikio. Na kundi hili lina watu wachache kwa sababu watu wengi wameng’angana’ katika makundi mengine ambayo nimekwisha yaelezea hapo awali.

Watu ambao ambao wapo  katika kundi hili huwa wanasifa zifutazo;

Wao hujua ni nini wanachokitaka katika maisha yao.

Wao hupanga na kukamilisha yale waliyoyapanga kwa wakati.

Lakini kubwa zaidi watu ambao wapo katika kundi hili huwa si wabinafsi kama walivyo makundi wangine, wao huwa wapo tayari kuwasaidia wengine.

Pia ni  watu ambao wamewekeza muda mwingi sana katika kujifunza na kutafakari.

Hayo ni machache kati ya mengi yaliyopo katika kundi hili.

Hayo ndiyo makundi matatu yaliyopo katika ulimwengu huu, Mara baada ya kuona makundi matatu ya watu yanayotufautisha hapa duniani. swali linakuja wewe mwenzangu na mimi upo kundi gani? 
Kama unahisi upo kundi ambalo hustahili, unachotakiwa kufanya ni kuhama mara moja na kuhamia katika kundi lenye mafanufaa kwako.

Asante kwa kuwa pamoja nasi kila wakati nikutakie siku njema na mafanikio mema.


HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment