Rais wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza waziri Suleimani Jafo kumfukuza kazi moja kwa moja mtumishi aliyechana Quran tukufu kilosa mkoani Morogoro.
Kauli hiyo ameitoa leo akiwa,Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akizindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.
“Juzi nilkuwa namsikiliza Waziri Jafo yupo Mtumishi alichana Quran nafurahi umemsimamisha kazi, lakini naagiza afukuzwe moja kwa moja, ashinde kesi asishinde ila aondoke, muandikie barua ya kumfukuza, akitoka huko atajua mwenyewe atakakoyatafuta Maisha”- JPM
No comments:
Post a Comment