Breaking

Saturday, February 22, 2020

Bora angefariki kabisa tu" - Nay Wa Mitego

Msanii Nay Wa Mitego amesema kiki aliyoifanya msanii Meja Kunta kuhusu kujizushia kifo ni bora angefariki kiukweli watu wangejua moja na kuendelea na mambo mengine kuliko vile alivyofanya yeye na uongozi wake.

Akifunguka hayo kupitia show ya Friday Night Live "FNL" ya East Africa TV inayoruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00  hadi 5:00 usiku, Nay Wa Mitego amesema amechukizwa na kitendo kile  kwa sababu Meja Kunta bado ni msanii chipukizi ila kwa kiki ile imempotezea mashabiki wengi.

"Niliangalia kiasi gani ile taarifa ilivyotoka na watu walivyoumia kuhusu yeye, watu walipata mshtuko bado alikuwa msanii mchanga, pia mimi ni mmoja wa watu ambao nilisafiri naye kwenye siku hiyo ya tukio lenyewe ambapo ndipo walidanganya kama wamepata ajali na nilikuwa najua kinachoendelea" ameeleza Nay Wa Mitego

"Hata mimi nilipomsikia meneja wake amesema ni kweli amefariki hata mimi nilipata mshtuko, ila baadaye nilipopata taarifa za chinichini kwamba ni mchezo wanatuchezea nikasema bora huko alipo afariki kiukweli kabisa, hata wale watu aliokuwa naye bora wangemzimisha" ameongezaHIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment