Breaking

Saturday, February 8, 2020

Fumbo la Mke wa Lutu na Sodoma na Gomora

Sodoma na Gomora

Sodoma na Gomorrah ni miji iliyokuja kuangamizwa kwa sababu wakazi wake walifanya kufuru ya starehe mpaka kumsahau Mungu kabisa....na kibaya zaidi ni ile dhambi ya kutenda kinyume na maumbile

Ndani ya miji ile akawepo mchamungu mmoja naye alikuwa Lutu...mweledi mnyenyekevu na msikivu sana.. Baba wa mke mmoja na mabinti wawili

Mungu alikasirika na kuamua kuiteketeza ile miji miwili.,lakini akaamua kumuokoa mtumishi wake Lutu na familia yake ila kwa sharti moja! Kwamba Lutu aondoke na familia yake kabla miji ile haijateketezwa lakini 'ATAKAYEGEUKA NYUMA' atageuka jiwe la chumvi

Kwanini kugeuka nyuma? Fumbo la Sodoma hilo! Mke wa Lutu aligeuka nyuma na akageuzwa kuwa jiwe la chumvi!je

naye alikuwa mteja

Lutu na mabinti zake hawakugeuka nyuma na wakaenda kuishi mlimani mpaka Lutu alipokuwa mzee kabisa!

Mabinti zake wakajiongeza wakaona baba anazeeka mama hayupo na sisi ni mabinti! Tusipofanya namna kizazi kitapotea

Makatengeneza mvinyo mkali wakampa mzee akanywa akalewa.....wakampa unyumba baba yao....wakashika ujauzito na kizazi kikaendelea(hakuna ubaya hapa!)

Kinachonitatiza kwanini Mungu alisema atakayegeuka nyuma atageuka kuwa jiwe la chumvi?
Leo ni jumatatu twendeni kazini..mambo mengine hayana majibu.

No comments:

Post a Comment