Breaking

Sunday, February 2, 2020

Ijue Misingi Hii Ya Fedha, Maisha Na Mafanikio Inavyofanya Kazi


Hakuna unachoweza kusema unakipata kwenye maisha yako kwa kubahatisha. Kila kitu unachopata kwenye maisha yako ni matokeo ya msingi ambao unakuwa umejiwekea. kama umejiwekea misingi mibovu, ujue utapata matokeo mabovu pia.

Ni matumaini yangu wewe uweze kujifunza misingi sahihi ya mafanikio yako ili uweze kufanikiwa. Ni misingi hii sahihi ya fedha, maisha na mafanikio, ndiyo ambayo mimi na wewe nataka tuifatilie kwenye somo hili na kujifunza jinsi ya kuifanyia kazi kila siku.

1. Kipato unachokipata si sawa na utajiri. Sio kile unachokipata ndio kinakufanya uweTAJIRI bali kile unachowekeza ndicho kinachokufanya uwe tajiri. Kosa kubwa wanalofanya wengi ni kuweka akiba na kuitumia kwenye mambo ambayo hayana uwezo wa kuwasaidia KUFANIKIWA.

2. Utafiti unaonyesha ni asilimia mbili tu ya wazee wanaofikisha miaka 65 ni hao ndio wanakuwa wako huru kifedha. Asilimia kubwa inayobaki wanabaki wakiwa na maisha magumu sana na ya kuteseka. Hutakiwi kuwa miongoni mwa kundi la watakaoteseka, badilika sana na kuanza kuwekeza.

3. Utajiri haujengwi kwa siku, utajiri unajengwa kwa idadi ya miaka. Unatakiwa kuwa mtulivu sana hasa pale unapoamua kujenga utajiri wako na hutakiwi kuwa na papara, tulia, weka mipango na utafanikiwa. Ila kama utautaka utajiri wa siku moja tu, ni ngumu sana kufanikiwa, unatakiwa kuwa na mipango ya muda mrefu.

4. Uchaguzi unao wewe kwenye maisha, kupanda na kusubiri mavuno au kuwa omba omba katika kile kipindi cha mavuno ambapo tayari kuna watu walipanda wakati wa nyuma.

5. Unachotakiwa kujiuliza, je, ukipewa nafasi ya kuishi miaka 90, utakuwa na pesa za kukuwezesha kuishi miaka hiyo au utategemea msaada kwa watoto wako na watu wengine, tafakari hilo kama utaona hutajiweza, kisha weka utani pembeni na ongeza juhudi sana za kutafuta pesa.

6. Moja kati ya kitu cha kushitua sana katika maisha ya siku hizi, kila mtu ukimuuliza kwamba ana mkopo sehemu, idadi kubwa sana watasema ndiyo. Utafikiri swali hilo umeuliza nani ni binadamu. Usijenge tabia sana ya kuazima pesa, jenga tabia ya kuazima watu pesa na si kuazima.

7. Haina haja ya kulalamika sana, unatakiwa ujifunze kwa bidii na hadi ukaelewa namna ya kuongeza pesa ulizonazo zikawa hata mara tano. Huhitaji wewe mshahara mkubwa. unachohitaji ni juu ya kujua jinsi unavyoweza kuongeza pesa ulizonazo na ukafanikiwa kwa asilimia kubwa.

8. Ikiwa leo maisha yako ya uzeeni yataishia kwenye umaskini, sio swala la kumlaumu Mungu. Unatakiwa kujilaumu wewe kwa kushindwa kwako kufanya uchaguzi sahihi wa kupanda katika kipindi cha kupanda na kuvuna katika kipindi cha mavuno na si kuwa ombaomba.

9. Mkakati wa kuwekeza kwa muda mrefu unatakiwa uwe na mambo haya yafuatayo:-
 Moja, wekeza kila mwezi, kwa muda usiopungua miaka 20 kutokana na kipato unachokipata bila kujali kipato hicho ni kidogo kiasi gani.

Mbili, wekeza kila mwezi bila kujali, huo mwezi ni una Tsunami, una maafa au mwezi una mafuriko ya kiasi gani. Ila unachotakiwa kufanya ni kuwekeza angalau kila mwezi kwa kile unachokipata, hakuna haja ya kutoa sababu au kisingizio chochote.

10. Ukitaka kujenga utajiri wako na ukafika mbali kweli, amua kuujenga utajiri wako kama kobe. Chukulia kama hizo ni mbio za muda mrefu, usikurupuke kujenga utajiri wako utakwama sana.

No comments:

Post a Comment