Breaking

Thursday, February 20, 2020

Iran: Black Box ya ndege ya abiria ya Ukraine imeharibika


Iran imesema Kisanduku cheusi (Black Box) cha ndege ya abiria ya Ukraine iliyodunguliwa kwa bahati mbaya na Iran mwezi uliopita kimeharibika na kiwanda cha Jeshi kimeombwa kukikarabati.

Iran imesisitiza kuwa licha ya kuharibika lakini imetafakari na kuona haina haja ya kukabidhi kisanduku hicho kwa nchi nyingine licha ya kulazimishwa kufanya hivyo na nchi nyingine kama Marekani na Canada ili zifanye uchunguzi.

Waziri mkuu wa canada Justin Trudeau amesema amemshauri Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif kuwa uchunguzi kamili na huru kuhusiana na kudunguliwa kwa ndege hiyo ni lazima ufanyike na Black Box ambayo ilirekodi data zote za safari za ndege hiyo ni muhimu kupatikana.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment