Breaking

Monday, February 10, 2020

Iran yasema imefanikiwa kurusha satelaiti yake

Iran imesema imefanikiwa kurusha satelaiti yake, lakini imeshindwa kuufikia mzingo wa dunia na hivyo kuwa pigo katika mpango wake ambao Marekani inasema unahusiana na makombora.

Uzinduzi huo umefanyika siku chache kabla ya maadhimisho ya miaka 41 ya Mapinduzi ya Kiislamu na uchaguzi muhimu wa bunge nchini Iran.

Mvutano wa muda mrefu kati ya Iran na Marekani uliongezwa kasi mwaka 2018 baada ya Rais Donald Trump kujiondoa kwenye mkataba wa nyuklia wa Iran, kabla ya kuweka masharti mapya kwa Iran kuachana na kutengeneza makombora ya masafa marefu. Iran imesema haina mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia na kwamba shughuli zake za anga ni salama na zinazingatia azimio la Baraza la Usalama la Umoja la Mataifa.

No comments:

Post a Comment