Breaking

Sunday, February 9, 2020

Jinsi ya kuondokana na tabia ya kulalamika katika maisha


Mara nyingi kama ikitokea afya yako haipo sawa, huwa unakunywa dawa ili kurudi katika hali yako ya kawaida.  kama ilivyo katika afya vivyo hivyo  katika safari yako ya mafanikio kama una tabia za kulalamika unahitaji dozi ya dawa ambayo itakufanya upone kabisa ugonjwa huo.

Najua utakuwa umeshangaa nilivyosema ni ugonjwa, wala usishangae, kulalamika katika maisha ni ugonjwa ambao watu wengi wamekuwa wakiuugua, na wengi wa watu hao wamekuwa hawajui ni dozi gani itawafaa ili waweze kupona, hivyo katika makala haya nitaueleza ni kwa jinsi gani utapona ugonjwa huo.

Ugonjwa wa kulalamika umekuwa kizuizi kikubwa katika kuyafikia mafanikio yako, unajua hii ipoje? Ipo hivi mafanikio ya kweli huanza kujengwa nafsini mwa mtu, kama itatokea ya kwamba unalalamika sana katika maisha yako ni lazima utajikuta huna amani ambayo itakufanya uweze kupata mafanikio.

Ukosekanaji wa amani katika nafsi ya mtu kwa namna moja ama nyingine hutengeneza kinyongo ndani yake na mtu ambaye analalamikiwa, na kinyongo hicho kinatakufanya usiweze kupiga hatua zozote za kimaisha.

Mara nyingi ukijaribu kuwachunguza watu ambao hulka na kalama yao kubwa ambayo ipo katika kulalamika maisha yao yapo katika mstari mwekundu wa kuelekea kufa maskini, Hii ni kwasababu ya licha ya watu hao kuendelea kulalamika wamekuwa hawachukui hatua zozote za kuwafanya wao wasonge mbele zaidi ya watu hao kuendelea kulalamika, ukiwauliza watu hao mara nyingi watakwambia serikari ndo chanzo, wengine watawataja ndugu na jamaa na marafiki ndiyo chanzo cha mambo yao fulani falani kutokuwa sawa.

Japo yawezekana ukaona hizo ni sababu na chanzo cha wewe kuwa hivyo ulivyo, kama ambayo kauli mbiu yetu ituongozayo katika kufanya kazi ya kwamba “badili maisha yako kwa kuwa fikra sahihi”, hivyo unachotakiwa kufanya kutumia dozi hii itayokusaidia kupona ugonjwa huo.

Dozi hiyo ni kukubalina na hali iliyotokea.

Ili kupona na ugonjwa huu wa kulalamika unachotakiwa kufanya ni kukubaliana na hali ambayo imetokea. Kama umefukuzwa kazi ambayo ulikuwa unaipenda basi kubaliana na hali hiyo, kama maisha yako ni magumu huku ukitoa sababu ya kwamba wewe ni yatima unachotakiwa kufanya ni kuacha kulalamika bali ni kukubalina na hali hiyo.

Yawezekana zipo sababu nyingine mbalimbali ambazo unazijua wewe zimekufanya umekuwa mlamikaji mzuri , ninachotaka kukwambia siku ya leo kulamikia sio dawa bali ni ugonjwa wa umasikini, hivyo ni vyema ukaacha tabia hiyo mara moja.

Hivyo jijengee tabia ya kutafuta majibu mengine ya malalamiko yako, na majibu yako hayo yawe chanya na yenye kukujenga katika kufikia mafanikio yako. Mwisho nimalize kwa kusema kama ambavyo vijana wasemavyo pambana na hali yako, nami nasema acha kulalamika pambana na hali yako kwani uwajibikaji wa mtu binafsi katika kuyasaka mafanikio ndiyo siri ya kufanikiwa kwako.

No comments:

Post a Comment