Breaking

Thursday, February 20, 2020

Liwale yauanza mwaka 2020 na mimba kumi kwa wanafunzi wa shule za sekondari


Na Ahmad Mmow, Lindi.

Wakati upimaji kwa wanafunzi wakike  wa shule za sekondari unaendelea wilayani Liwale, wanafunzi kumi wamebainika kuwa wana mimba.

Hayo yameelezwa na mkuu wa willaya hiyo, Sarah Chiwamba, jana alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Liwale.

Chiwamba alisema baada ya kufunguliwa shule za msingi na sekondari wilayani humo mwaka huu( 2020) katika muhula wa kwanza wa masomo, wanafunzi 10 miongoni mwa walipimwa katika shule za sekondari  wamebainika kuwa wana mimba.

Mkuu huyo wa wilaya ya Liwale ambae aliweka wazi kwamba hayo ni matokeo ya awali tu, kwani zoezi la upimaji linaendelea aliitaja shule ya sekondari ya kutwa ya R.M. Kawawa imekuwa kinara katika matokeo ya upimaji huo. Kwani hadi sasa wanafunzi wake wanne kati ya hao kumi wamebainika kuwa wana mimba.

" Katika jitihada za kutomeza tatizo la mimba za utotoni tumeanzisha klabu shuleni.Ni utaratibu tuliojiwekea kwamba wanafunzi wanaporudi shuleni baada ya kumalizika likizo wanapimwa. Katika upimaji unaondelea imegundulika wanafunzi kumi wana mimba," alisema Chiwamba.

Alisema haitashangaza iwapo idadi ya wanafunzi wenye mimba itaongezeka. Kwani upimaji huo unaendelea katika shule za sekondari zilizopo wilayani humo.Hata hivyo anatarajia kiwango cha tatizo hilo kinaweza kupungua kutokana na mikakati mbalimbali iliyopo ya kukabiliana nalo.

Chiwamba alisema katika kukabiliana na tatizo hilo wameanzisha klabu shuleni, ambazo zitasaidia kutoa elimu.Lakini pia watoto wakike kujengewa uwezo wa kujiamini na kuamini wanaweza kutimiza ndoto zao kielimu kama watoto wa kiume.

 Alitoa wito kwa wazazi,walezi na jamii kwa jumla wilayani humo washiriki kikamilifu katika vita dhidi ya mimba na ndoa za utotoni ili watoto wakike wafikie ndoto zao badala ya kukatizwa na watu ambao hawajui umuhimu wa elimu kwa watoto hao wa kike.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment