Breaking

Thursday, February 20, 2020

Makubwa...Dada Watano Wampiga Kaka yao Hadi Kufa Kisa Mbuzi wa Mahari

Polisi wa Kaunti ya Kiambu nchini Kenya wanachunguza kifo cha Paul Njeri (51), ambaye anadaiwa kupigwa na Dada zake watano hadi kumuua baada ya kudai apewe mbuzi aliyetolewa kama mahari kwakuwa yeye ndiye mkubwa

Ugomvi baina ya Wanafamilia hao ulianza baada ya Mama yao kusema Mjomba anastahili kupokea mbuzi huyo, kwakuwa tamaduni zao haziruhusu Wanawake ambao hawajaolewa kupokea mahari

Baada ya Njeri kupinga uamuzi huo, Dada zake Susan Wambui, Elizabeth Wairimu, Catherine Wanja, Alibeta Njambi na Mary Muthoni kwa pamoja walimpiga na walipokuja kumuangalia asubuhi yake walikuta amefariki dunia

Ndugu hao watano wanashikiliwa na Polisi na uchunguzi wa kifo cha Kaka yao unaendelea.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment