Breaking

Thursday, February 27, 2020

Mama Akamatwa Kwa Kuolewa na Wanaume Wawili

Mwanamke mmoja mweye watoto 7 ambaye amejulikana kwa jina la Hauwa Ali (37), mkazi wa Mariri kaskazini mwa nchi ya Nigeria, amekamatwa na Polisi kwa kosa la kuolewa na wanaume wawili tofauti.

Afisa Mahusiano na Umma wa jimbo la Kano Alhaji Lawan, akitoa ripoti ya taarifa hiyo amesema,

 "Mwanamke huyu alikuwa katika ndoa na mwanaume wa kwanza wake aitwaye Bello Ibrahim (45), ambaye alikuwa anaumwa kwa muda mrefu hadi akahamishwa kupelekwa kijijini kwa ajili ya matibabu ambapo mwanamke huyo alidhani amefariki".

Pia  Alhaji Lawan ameendelea kusema "Kisha aliamua kuolewa na mwanaume wa pili aitwaye Bala Abdulsalam (40), ambaye alimtolea mahari ya Tsh 126,580 na alidai kuwa amepewa talaka na mwanaume wa kwanza".

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment