Breaking

Thursday, February 20, 2020

Mamake Diamond Anamtaka Sasa Mwanawe Amuoe Tanasha na Kuwatema Warembo Wengine


- Mama Dangote amemuhimiza mwanawe kumuoa Tanasha kwani ndiye chaguo bora

- Mama huyo alitoa matamshi hayo huku akimumiminia Tanasha sifa kwa kibao chake kipya

- Wapenzi hao walijibu ujumbe wa Mama Dangote huku Tanasha akikubaliana na mama mkwe wake naye Diamond akiahidi kufuata ushauri wa mama yake

Mama ya msanii Diamond amemshauri kuingia katika ndoa kwa kumuoa mpenzi wake wa sasa ambaye pia ni mama mtoto wake, Tanasha Donna.

Huku akimiminia sifa kibao chake kipya akimshirikisha Tanasha kwenye Instagram, Mama Dangote alimuomba mwanawe kuachana na mtindo wake wa kuwabadilisha wanawake na kumfanya Tanasha kuwa mke wake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

Mama Dangote alimuelezea Tanasha kama chaguo bora kwa mwanawe na kuongezea kuwa anatakiwa kuwatema wanawake wengine.

 "Umepata sasa Diamond na sasa tulia, achana na wanawake wengine," alisema Mama Dangote kuhusianana kibao chao kipya cha Gere.

Jambo la kushangaza ni kuwa, Tanasha alijitosa kwenye sehemu ya maoni na kuunga mkono matamshi ya mama mkwe wake kwa kusema "mama ameongea."

Diamond pia alijitokeza na kuahidi kufuata ushauri wa mama yake kwa kukiri kuwa tayari amewabwaga wanawake wengine. "Nimewachana nao mama," aliandika Diamond.

Basi huenda staa huyo wa Bongo Flava ambaye aliahidi kumuoa mrembo huyo wa Kenya mwaka huu akawa na presha.

Wakati wa harusi ya dada yake, Queen Darleen mwishoni mwa mwaka 2019, Diamond katika mahojiano na Wasafi TV alisema anatazamia kufanya harusi na Tanasha mwaka 2020.

Mwimbaji huyo wa wimbo Baba Lao alisema Tanasha anamtosheleza na hana sababu yoyote ya kukosa kumfanya kuwa mke wake.

HIZI HABARI ZA HIVI ZINAPATIKANA GODSTAR ONLINE >>BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD APP YA GODSTAR ONLINE

No comments:

Post a Comment