Breaking

Monday, February 10, 2020

Mambo ambayo wanawake wengi hudanganya wanapoingia kwenye mahusiano
Umri

Wanawake wengi wanaamini wanaume wanavutiwa na wanawake wenye umri mdogo, wanawake walio na miaka kati ya 24-29 mara nyingi huwa wanashusha miaka 2 hadi 3 ili waonekane wadogo mbele ya wanaume.

Kutokuwa na Mahusiano
Baadhi wa wanawake, husema wapo kwenye mahusiano hata kama hawapo,hii inatokea hasa kama mwanamke hamtaki mwanaume aliemtokea wakati huo na kisingizio kikubwa ni yeye kuwa katika mahusiano na huu ni uongo mmoja maarufu sana na baadhi ya wanawake pia huwa wanaficha kama wapo kwenye mahusiano, hasa pale wanapotaka kuanzisha mahusiano mapya, huku wakiendelea kuwa na mahusiano na wanaume wawili kwa wakati mmoja.

Mara ya mwisho kukutana kimwili na mwanaume
Mwanamke hawezi kukwambia ukweli kuhusu hili hata kama alikutana na mtu kimwili jana, atakwambia miezi 4-8 iliyopita, hii ni kwasababu anaona ataonekana muhuni sana au malaya, na wengi wao huwa wanataka kuonekana wasafi au tuite watakatifu. Kitu ambacho sio cha kweli hata chembe.

Ameshakuwa na wapenzi wangapi
Uongo mwingine ambao ni maarufu ni kuhusiana na wanaume wangapi ametoka nao, hapa sahau sana kwani huwezi kupata jibu sahihi, sababu wanawake wengi huwa wanadanganya mahusiano yao ya nyuma, anaweza kukwambia wawili au watatu kitu ambacho inaweza kuwa zaidi ya hao. Japokuwa uongo huu hata wanaume pia wanadanganya.

Kudanganya kuhusu vitu alivyozoea
Wapo wanawake wanadanganya kuhusu kutoka usiku, labda sio watu wa tungi/Gambe, sio watundu kitandani na kujidai ndo kwanza mambo wanayaanza siku hiyo. Kujidai hawawezi hiki mara kile mara akwambie mie ndo mara yangu ya kwanza ilimladi vituko .

Ila kitu kimoja ambacho nimegundua mwanamke mpaka anafikia stage ya kudanganya haya ni kwa sababu ana mapenzi ya dhati na mtu huyo na anaogopa kumpoteza kama akijua baadhi ya vitu vyake vya ndani. Japokuwa wakati mwingine hali hii haijengi bali inabomoa mahusiano.

Kabila lake.
Mara nyingi mahusiano yanapoanzishwa kwa mara ya kwanza ni rahisi sana mwanamke kudanganya kabila lake, hii ni kwa sababu wengi huwa wanaona kama mwanaume anaweza kughairi kuwa naye hii ni kutokana na tabia zilizopo kwenye kabila husika.

No comments:

Post a Comment