Breaking

Monday, February 10, 2020

Mambo ya kuzingatia ili kufanya biashara yenye faida endelevuIli uweze kufanya biashra yenye muendelezo na faida lukuki unatakiwa kuelewa kanuni muhimu sana za kuweza kuwa hivyo.

Yafuatayo ndiyo mambo ya kuzingatia ili uweze kufanya biashara yenye yenye faida endelevu;

Kuwa makini toka mwanzo kujua nani haswa watakua wateja wa biashara yako.

Chunguza kweli kweli nini haswa watu wanataka katika soko. Usikubali tuu kutengeneza bidhaa kwa sababu wewe unapenda kufanya hiyo product. Ingawaje uzuri na ubora wa kitu ni muhimu katika kuuza bidhaa, lakini kama si kitu ambacho mtu anakihitaji hatonunua.

Jiwezeshe kweli kweli katika ufahamu wa utengenezaji wa hiyo bidhaa yako. Kwani watu hawataki tuu bidhaa ili mradi , na kama unataka kutoka haswa basi inabidi uwe na kitu special cha kuwapa watu.

Jifunze kuhusu masoko na kujitangaza. Uwe makini na social media, fikiria namna gani unataka kujitambulisha katika jamii ili kweli watu wakukubali.

Anza sasa kujionyesha kupitia mtandao, na hata nje ya mtandao kuwa mtu unayejiheshimu na unayeweza kuaminika kwani ili uweze kuwauzia watu inabidi kwanza wakuamini na kutazamia mazuri toka kwako.

Usisubiri mpaka mambo yakae vema kama unavyofikiria kichwani mwako eti  uanze kujaribu hiyo biashara. Wapo wengi huwa na mawazo mazuri lakini hawaanzishi biashara kwakua  wanajiwekea vikwazo vingi wao wenyewe, vikwazo ambavyo  havina msingi kwakua biashara inahitaji sana kujaribu.

Ukishajua bidhaa gani unataka kutengeneza, umeshatambua nani haswa unawalenga kuwauzia , anza mara moja kidogo kidogo, usiwaze kutaka kuanza biashara katika kiwango kikuubwa.

Mara kwa mara biashara hukua baada ya kujifunza mambo madogo madogo , na kuwa na imani kuwa mambo yataenda sawa. La msingi ni kujifunza, uwe na subira na ujue kuwa katika biashara swala sio kupata mapato swala la msingi ni kutimiza mahitaji ya watu na kujifunza kujiboresha siku hadi siku. Ukiingia katika biashara kwa lengo la kutaka “kupiga hela” uishie zako,  unaweza jikuta upo katika wakati mgumu sana.

No comments:

Post a Comment